![]() | |
|
WAZIRI
Mkuu, Kassim Majaliwa amekatisha ziara yake ya siku sita mkoani Simiyu,
baada ya kifo cha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa (DED),
Trasias Kagenzi kilichotokea juzi usiku.
Kaimu
Katibu Tawala, Donatus Weginah alithibitisha kutokea kifo cha mkurugenzi
huyo wakati Waziri Mkuu akiwa na ratiba ya kutembelea wilaya hiyo.
Weginah
alisema juzi asubuhi Kagenzi alikuwa akifanya mazoezi ya kukimbia akiwa
na mlinzi wake na Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Rosemary Kirigini lakini
alianza kujisikia vibaya.
“Mkurugenzi
alikuwa akifanya mazoezi ‘jogging’ na DC Rosemary Kirigini, lakini
baadaye alimwambia Kirigini najisikia pumzi zinabana, akamwambia
aendelee… lakini mara mkuu wa wilaya alimuona amejiinamia, aliporudi
kumuuliza akamwambia naona nakosa hewa, ndipo alipoamua kukimbia
kuchukua gari kumpeleka hospitalini,”alisema.
Weginah
alisema mkurugenzi huyo alipelekwa hospitali na majira ya saa tano
asubuhi alionekana akiendelea vizuri, hata hivyo baadaye hali
ikabadilika mchana na waliamua kumpeleka katika Hospitali ya Bugando kwa
uchunguzi zaidi, lakini usiku wa saa saba alifariki dunia.
Kwa
mujibu wa Kaimu Katibu Tawala huyo, alisema mkurugenzi ana kama mwaka
mmoja na nusu tangu alipohamia wilayani humo na kwamba familia yake iko
Arusha.
Weginah
alisema jana mchana mwili wa Kagenzi ulichukuliwa hospitalini Bugando na
kuletwa wilayani Maswa ambapo leo asubuhi Waziri Mkuu Majaliwa
ataongoza kuaga mwili wa mkurugenzi huyo.
CHANZO MAGANGAONE
CHANZO MAGANGAONE

Post a Comment