Mkuu
wa Mkoa wa Singida, Mathew Mtigumwe ameagiza mamlaka zinazohusika
kuwakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria watu watakaobainika
kutafuna fedha za mishahara hewa kabla ya mwezi huu kumalizika.
Mkuu
huyo wa mkoa alitoa agizo hilo juzi kwenye kikao cha kufahamiana
kilichohudhuriwa na wakuu wa wilaya, wakuu wa idara ya sekretarieti ya
mkoa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa ofisini kwake.
Katika
hotuba yake fupi na ambayo haikuwa na mbwembwe za kisiasa, alisema
uhakiki uliofanyika hivi karibuni mkoani humo ulibainika kuwa na
wafanyakazi hewa wengi, jambo linaloonyesha kuwapo kwa ubadhirifu wa
kiwango cha juu cha fedha za umma.
“Naagiza
kila mmoja wenu akaangalie kwenye taasisi yake iwapo wafanyakazi
wanaolipwa mishahara ndiyo hao waliopo kazini au la. Kuna madai
wastaafu, waliohama na hata watumishi waliokufa mishahara yao bado
inalipwa hadi hivi leo,”alisema.
“Iwapo
itagundulika kuwa kuna watu walioshiriki katika ulaji huo wa fedha za
umma, wakamatwe mara moja ifikapo Aprili Mosi, mwaka huu na kufikishwa
kunakohusika haraka iwezekanavyo ili sheria ichukue mkondo wake.”
Mtigumwe
aliwakumbusha viongozi hao umuhimu wa watumishi walio chini yao kufanya
kazi kwa uadilifu na kujiepusha na vitendo vya rushwa.
“Haiwezekani mtu atoke kijijini kisha arudi bila kuhudumiwa, lazima kuwahi kazini na kukaa hadi mwisho wa saa za kazi,” alisema.
Post a Comment