Mkoa wa Dar es Salaam ni miongoni mwa majiji yanayoongoza kwa uchafu Tanzania.
Siku
chache zilizopita Rais Magufuli alifanya uteuzi wa wakuu wapya wa
Mikoa, aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda aliteuliwa
kuwa mkuu mpya wa mkoa wa Dar es Salaam.
Baada
ya uteuzi huo na kuapishwa ikulu, Makonda alifanya mkutano kwenye
ukumbi wa Mwalimu Nyerere ambao uliwajumuisha wenyeviti wote wa mkoa wa
Dar es Salaam na wadau wengine wa maendeleo.
Agenda
ya uchafu ndiyo ilishika nafasi kubwa kwenye mkutano huo. Mh Makonda
aliwataka wenyeviti wote wa mkoa wa Dar es Salaam kuanza usafi kwenye
mitaa yao, pia aliahidi kutoa zawadi ya gari lenye thamani ya shilingi
milioni 20, na zawadi ya pikipiki kwa wajumbe wake ambao mitaa yao
itaonekana ni misafi.
‘Kidole
kimoja hakivunji chawa’, ushirikiano pekee na umoja ndiyo unaweza
kufanikisha hili kutimia. Vijana wengi wapo mitaani wanalalamika hakuna
ajira, lakini kwa hili inaweza ikawa neema na fursa pekee ya ajira kwao.
Vijana
wanaweza kuunda vikundi vyao kwa ajili ya kufanya usafi kwenye mitaa
yao na kuweka unlizi kwa pamoja, siamini kuwa kama kutakuwa na mwenye
muda kila siku wa kufanya usafi na kumsimamia mwenzake kwenye hili.
Viongozi
wa serikali za mitaa na wananchi wao wanaweza kupanga kuchangishana
fedha fulani ili kuwapatia vijana hao ambao watakuwa wanafanya usafi na
ulinzi kwenye mitaa yao. Hakuna kiongozi anayeweza kukutafutia kazi, ila
anakutengenezea misingi ya kuweza kujiajiri mwenyewe kama hili
lililotokea sasa.
Post a Comment