Wafanyakazi katika kiwanda cha kutengeneza Vibiriti cha Alfa Match
kilichopo Mbagala jijini Dar es salaam wamegoma kufanya kazi kwa madai
mbali mbali ikiwemo kutokuwapo kwa mikataba ya kazi kwa zaidi ya miaka
10, lugha chafu kutoka kwa mwajiri wao pamoja na malipo kidogo licha ya
kufanya kazi ngumu na kwa muda mrefu.
Wafanyakazi hao huku baadhi yao wakiwa na mabango wamesema wengi wao wamefanyakazi kwa zaidi ya miaka kati ya 10-12 lakini hawajapewa mikataba ya ajira huku mwajiri akitumia mwanya huo kuwafukuza pindi wanapodai mikataba ya kazi.
Wamedai wamekuwa wakifanya kazi kwa muda mrefu, kutolipwa malipo ya ziada, na kuongezewa shilingi hamsini tu, ambapo kwa siku wamekuwa wakilipwa shilingi 3650 tu hali waliyodai ni dharau kwao.
Muda mfupi baadaye, Mkuu wa wilaya ya Temeke Sophia Mjema alifika eneo hilo kwa lengo lam kusikiliza malalamiko ya wafanyakazi hao ambapo aliingia ndani ya kiwanda hicho ili kuonana na uongozi wa kiwanda, huku meneja wa kiwanda hicho akikataa kata kata waandishi wa habari kuingia kiwandani mpaka pale alipotishiwa.
Katika hali isiyokuwa ya kawaidia kiwanda hicho chenye wafanyakazi zaidi ya 3500 hakina meneja rasilimali watu-au HR ambapo baada ya Mkuu wa wilaya huyo kumuhitaji, Meneja wa kiwanda alimleta mfanyakazi ambaye alimpachika cheo hicho ghafla, ambapo baada ya kuhojiwa alikiri kupewa cheo hicho ghafla.

Post a Comment