Kocha mkuu wa timu
ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa ametangaza
kikosi cha wa wachezaji 25 kwa ajili ya mchezo wa kuwania kufuzu kwa
fainali za mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya Chad.
Mechi hiyo imeratibiwa kusakatwa tarehe 23 Machi mjini Djamena.Wachezaji walioitwa Taifa Stars ni magolikipa Aishi Manula (Azam FC), Ally Mustapha (Young Africans) na Shaban Kado (Mwadui FC), walinzi ni Juma Abdul, Haji Mwinyi, Kelvin Yondani (Young Africans), Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, David Mwantika (Azam FC) na Mohamed Hussein (Simba SC).
Washambuliaji ni Nahodha Mbwana Samatta (KRC Genk), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe), John Bocco (Azam FC), Elias Maguri (Stand United), Jeremia Mgunda (Tanzania Prisons) na Ibrahim Hajibu (Simba SC).
Post a Comment