Uchaguzi
Mkuu wa Tanzania ulifanyika huku baadhi ya majimbo ya uchaguzi, uchaguzi
uliahirishwa kutokana na kuwepo kwa sababu mbalimbali. Tume ya Uchaguzi
iliteua jumla ya Wabunge wanawake wa viti maalum 110 kati ya 113 ambapo
viti vitatu vilibakizwa kusubiri uchaguzi wa majimbo nane ambayo
uchaguzi wake uliahirishwa.
Chama cha
Mapinduzi ‘CCM’, Chama cha Demokrasia na Maendeleo ‘CHADEMA’ na Chama
cha Wananchi ‘CUF’ ndivyo vimetajwa kuendelea kuhusishwa kwenye mchakato
wa kugawanywa viti 3 vilivyobaki kutokana na kupata angalau asilimia 5
ya kura halali za ubunge.
Leo March 24 2016 Tume ya Taifa ya Uchaguzi ‘NEC’ imewateua ndugu Ritha Enespher Kabati na Oliver Daniel Semuguruka wa Chama cha Mapinduzi ‘CCM’ na ndugu Lucy Fidelis Owenya
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ‘CHADEMA’ kuwa wabunge Wanawake wa
viti Maalum katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Uteuzi huo
umefuata mtiririko wa orodha iliyowasilishwa na katibu wa Chama husika
ambapo CCM iliwasilisha majina nambari 65 na 66
65.Ritha Enespher Kabati
66.Oliver Daniel Semuguruka
Katika Orodha iliyowasilishwa na CHADEMA jina nambari 37
37. Lucy Fidelis Owenya
Post a Comment