Je, unaikumbuka
siku za Nokia na enzi zake? Jina Nokia linatokaka na mji mdogo nchini
Finland, ambapo simu hiyo iliyokuwa maarufu duniani iligunduliwa.
Wakati ikiwa katika kilele chake kwa mapema miaka ya 2000, Nokia iliuza asilimia 40 ya simu zote duniani ambapo ilitambuliwa na kuwa simu maarufu zaidi duniani.
Nchini Finland kwenyewe matokeo yalikuwa hata
makubwa. Kulingana na taasisi inayofuatilia uchumi wa Finland ni kuwa
simu za Nokia zilichangia robo ya uchumi wa nchi hiyo kati ya mwaka 1998
na 2007.
Wakati wa kilele chake, iliwaajiri zaidi ya watu 4,000.
Lakini kwa ghafla soko la simu za Nokia lilishuka kwa kishindo na mauzo kudorora kabisa hali hiyo iyoathiri pakubwa uchumi wa Finland na pia kusabibisha kuwepo kipindi kigumu na kirefu kwa uchumi wa nchi hiyo.
"Nokia ilikuwa ni uti wa mgongo wa kila kitu hapa, kuanguka kwake ilikuwa ni kama jinamizi kwa taifa la Finland kwa mujibu wa mkurugenzi wa uchumi na maendeleo ya mji wa Tampere, Kari Kankaala, mji ulio umbali kidogo kutoka Nokia.
Nokia iliathiriwa sana na kubadilika kwa teknolojia ya simu.
Ilijipata katika njia panda hasa kutokana na kutokea kwa simu aina ya smartphone, na hasa kuzinduliwa kwa simu ya iPhone na kampuni ya Apple mwaka 2007.
Meneja wa zamani wa utafiti wa ustawi katika Nokia Mika Grundstrom anasema kampuni hiyo kwa kiasi kikubwa ilikabiliwa na kizungumkuti.
"Mambo yalianza kuwa magumu. Hatukujua tulifaa kuangazia nini. Tuangazie urahisi wa kutumia simu, kudumu kwa betri au ukubwa wa simu?," anasema.
"Ukifikiria kuhusu betri, tulikuwa na simu zingedumu na moto wiki nzima. Kisha, una simu hii mpya yenye nguvu sana ambayo unahitaji kuichaji kila siku. Sasa utaitangaza vipi kwa mteja?"
Kampuni ya Nokia ilinunuliwa na kampuni ya Microsoft mwaka 2014.

Post a Comment