Dar es Salaam, Tanzania
– February 29, 2016: Mwimbaji anaekuja kwa kasi kwenye muziki wa kizazi
kipya (Bongo Fleva) kutoka Tanzania anayewakilisha kundi la Wasafi
Classic Baby(Wcb),Harmonize ameachia wimbo wake wimbo mpya unaoitwa ‘BADO’ aliyomshirikisha Diamond Platnumz.
SABABU YA KUREKODI WIMBO HUU.
Kwa
singo mbili alizosikika Harmonize(Aiyola,Kidonda Changu) kwenye vyombo
vya habari,jamii imekua ikimfananisha sana na Diamond kwenye
uimbaji,ndipo siku moja Harmonize wakati akiimba Diamond alivutiwa na
Melody ya wimbo huu na kusema hii itakua nafasi ya Watanzania
kuwatofautisha kwenye uimbaji.
KUHUSU WIMBO WA BADO.
Harmonize
alikaa na Diamond akamuuliza ni msichana gani alishamuumiza kiasi
kwamba hawezi kumsahau,ingawa Diamond hakumwambia ni msichana
gani,lakini akamwambia hiyo ni idea(Mwanga) mzuri wa kutunga wimbo
‘mkali’ Beat ya wimbo huu imetengenezwa na Mtayarishaji(Producer)
anaitwa Fraga na kabla ya kurekodi kwenye studio ya Wasafi,producer
Fraga alimtumia midundo (Beat) 3 Harmonize achague,ndipo akachagua beat
ya wimbo huu na kurudi Wasafi Records kwa ajili ya kurekebishwa na
kuanza kurekodiwa.
VIDEO YA WIMBO WA BADO.
Video
ya wimbo huu imefanyika Afrika Kusini na Muongozaji(Director) anaitwa
Nick ambaye ametengeneza video kadhaa ikiwemo Aiyola ya Harmonize
mwenyewe,Make Me Sing ya Aka na Diamond,Love Boat Kcee na.Diamond,Walk
it off ya Fid Q na nyingine nyingi.
Note:Wimbo wa BADO na interview ya Harmonize vimeambatanishwa kwenye barua pepe hii.
Post a Comment