Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto,Dk Hamis Kigwangalla,amewataka wawekezaji nchini
hususani wanaojihusisha na biashara ya chakula,kuwapa kipaumbele
wajasiriamali wadogo na wa kati kwa kununua bidhaa zao badala ya kununua
bidhaa kutoka nje ya nchi.
Dk Hamis Kigwangalla,ametoa angalizo hilo jijini Dar Es Salaam,alipokuwa akizindua Supermarket inayofahamika kwa jina la Maisha,ambapo amesema,haiingii akilini kuona bidhaa za nje zinauzwa katika Supermarket husika wakati bidhaa hizo zinazalishwa hapa nchini,aidha,ametoa wito kwa wawelezaji hao,kuweka pia kipaumbele afya za Watanzania kwa kuuza bidhaa zisizokuwa na shaka yoyote juu ya usalama wa afya za walaji.
Awali Mkurugenzi wa Maisha Super Market,ABDILLAH GULED,alitoa wito kwa wajasiraimali kuchangamkia fursa kwa kupeleka bidhaa zenye ubora katika Supermarket hiyo waweze kunufaika na uwekezaji huo.

Post a Comment