Meneja wa timu ya
taifa ya Italia Antonio Conte ametangaza kwamba ataondoka kwenye wadhifa
huo baada ya kumalizika kwa fainali za taifa bingwa Ulaya 2016.
Conte
amehusishwa na nafasi ya umeneja iliyo wazi Chelsea na tangazo lake
litaongeza uwezekano kwamba huenda akahamia Stamford Bridge.Mkufunzi huyo wa umri wa miaka 46 aliteuliwa meneja wa timu ya taifa ya Italia Agosti 2014 muda mfupi baada ya kujizuulu wadhifa wake kama kocha wa Juventus.
"Anahisi kwamba anahitaji kuwa uwanjani zaidi, kuongoza mazoezi kila siku,” Rais wa Shirikisho la Soka la Italia Carlo Tavecchio amesema.
Conte aliongoza Juventus kushinda mataji matatu ya Serie A mtawalia kabla ya kuchukua kazi timu ya taifa.
Chelsea walimfuta kazi meneja wao Jose Mourinho Desemba 2015 na wakamteua Guus Hiddink kuwa kaimu meneja hadi mwisho wa msimu.
Post a Comment