Ikiwa
ni tunzo ya 4 tangu kuanza kwa zoezi la kumchagua mchezaji bora wa
mwezi ambapo zoezi hili lilianzishwa mwezi Septemba, 2015 likiwa na
dhumuni la kuongeza morali na kuwazawadia wachezaji wanaofanya vizuri.
Mshambuliaji
Ibrahim Ajibu ameshinda kwa mara ya pili tuzo ya mchezaji bora mwezi
Januari, 2016 baada ya kupigiwa kura kwa wingi na wanachama, mashabiki
na wapenzi wa Simba na soka la Tanzania kwa ujumla kupitia simu za
mkononi ambao pia wamejiunga na huduma ya Simba News pamoja na kwenye
mitandao rasmi ya kijamii ya Simba
Facebookwww.facebook.com/simbatanzania Twitter na Instagram @simbasctanzania.Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Rais wa Simba Evans Aveva amesema, “sisi kama uongozi wa klabu yetu ya Simba tunaamini katika kuwapa motisha wachezaji wetu kila iitwapo leo na hii ni katika kuongeza chachu ya maendeleo si tu kwa mchezaji bali kwa klabu nzima kwa ujumla, Ajib anashinda tunzo hii kwa mara ya pili mfululizo. Wote mtakubaliana nami kuwa kwa kiwango anachoonesha mshambuliaji Ajib ni kweli mshabiki, wanachama na wapenzi wa Simba hawajakosea kumchagua tena mchezaji huyu”Napenda kutoa wito kwa wachezaji wetu wote kuendelea kujituma zaidi kwani mashabiki wao wakiongozwa na uongozi mzima tunamatumaini makubwa msimu huu 2015/2016, tukiamini kwenye falsafa yetu ya SIMBA NGUVU MOJA, aliongeza Rais Evans Aveva.

Akizungumza
na simbasports.co.tz Mkurugenzi Mkuu wa EAG Group ambao ni washauri na
watekelezaji wa Masoko na Biashara wa Simba, Imani Kajula amesema, “EAG
Group inapenda kusisitiza kuendelea kuongeza utayari wake katika
kushirikiana na klabu ya Simba kwenye kutoa motisha kwa wachezaji wa
Simba ambapo italeta chachu ya kufanya vizuri zaidi na hivyo kuweza
kutengeneza mfumo mzuri wa kuongeza vyanzo vya mapato na hatimaye faida
kubwa kwa wachezaji na timu kwa ujumla”.
Simba
News ni huduma iliyoanzishwa na Simba ili kuwapa wapenzi wa Simba
habari mbalimbali za Simba popote pale walipo ikiwemo matokeo, majina ya
wachezaji wanaocheza mechi, usajili na habari nyingine za klabu ya
Simba. Kujiunga na Simba News tuma neno Simba kwenda namba 15460 kisha
utaletewa ujumbe jibu kwa kutuma neno “OK” na hapo utakuwa umejiunga
rasmi, Huduma hii ni maalum kwa Tigo na Vodacom.
Post a Comment