0



Na Mwandae Mchungulike
LIWALE-LINDI
Gari ya jeshi la Polisi lenye namba PT 3704  Land cruiser (mpya) la kituo cha polisi wilayani Liwale mkoani Lindi limeacha njia na kupinduka  na kujeruhi watu 6 maeneo ya kata ya Mungurumo tarafa ya Liwale mjini katika barabara ya Kichonda majira ya saa 8 mchana february 2 leo . 
Gari hiyo ikiwa inatoka katika kijiji cha Kimambi kumchukua mke wa askali Muddy ambaye alilala njiani tangu jana akiwa kwenye basi akitokea jijini Dar es salaam baada ya basi hilo kukwama umbali wa kilometa 40 kufika Liwale mjini,ilipokaribia kuingia mjini gari iliteleza na kuacha njia kisha kupinduka na kusababisha majeruhi ya watu 6 waliokuwa wameomba msaada kwenye gari ambao wamepata majeraha na michubuko sehemu mbalimbali ya miili yao.
Kamanda wa polisi wilaya ya Liwale Raphael Mwandu amesibitisha kutokea kwa ajali hiyo na alisema majeruhi  wamepatiwa matibabu na hali zao wanaendelea vizuri.
Kamanda Mwandu amewataja waliojeruhiwa katika ajali hiyo ni askali na dereva wa gari hiyo Desdery (45),Ubaya Kandros Mwingira (32) dereva na mkazi wa Kata ya Nangando liwale mjini,Ramadhani Saidi Kaselewenje (23) mkulima na mkazi wa Keko-Dar es salaam,Hassani ALLY Ponela( 26) mfanyabiashara na mkazi wa Dar es salaam,Ally Mussa Ahmad mfanyabiashara na mkazi wa uwanja wa ndege Dar es salaam na Shabani Othmani Lugume (40) mfanyabiashara na mkazi wa Kongowe Dar es salaam.
Pia kamanda huyo alisema gari hilo baada ya kupata ajali bado zima ila kioo cha mbele kimepata nyufa. 

         
   KUANGALIA TASWIRA YA BARABARA YA LIWALE TO NANGURUKURU>>> BOFYA HAPA 

Post a Comment

 
Top