
Timu ya Transporter yenye jezi nyeupe Vs Liwale Star
Chama cha mpira wa miguu wilaya ya liwale (lidifa) mkoani Lindi kimeandaa bonaza kwa lengo la kuzijengea uzoefu timu zitakazo shiriki ligi daraja la 3 ngazi ya mkoa timu tatu kutoka wilani hapa ni Liwale star,Liwale United na New Generation
Bonaza lilianza ufunguzi wake jana kwa mchezo kati ya timu ya New Genration vs Liwale united katika mchezo huu katika kipindi cha kwanza New Generation ilikuwa inaongoza kwa goli 2 kwa 1
Katika kipindi cha pili New Generation iongeza goli 2 na mpaka mpira unaisha dakika 90 matokeo yakawa New Genration 4 vs 1 Liwale united.
Leo ilikuwa katika uwanja wa wilaya ya Liwale ilikuwa zamu ya timu ya Transporter Vs Liwale Star Mchezo uliokuwa wa aina yake na kivutio cha mashabiki wa soka katika kipindi cha kwanza timu ya Liwale Star ilikuwa inaongeza bao 1 na kupelekea kudumu goli hilo mpaka mapumzi.
Katika kipindi cha pili Liwale Star iliongeza goli la pili huku timu ya Transporter ikijaribu kuhahaa kutafuta goli la kufutia machozi lakini aliambulia kutika bila bao la kufutia machozi mapaka mpira unamalizika matokeo yalikuwa Transporter 0 Vs 2 Liwale Star.
Mwandishi wa Pride fm-Mtwara na Liwale Blog iliongea na nahodha wa timu ya liwale star uwesu mbala juu ya mchezo huo "nashukuru mchezo tumemaliza salama na kuweza kushinda bao 2 kwa 1 tunashukuru kwakuwa ni mchezo wetu wa kwanza na sisi tulikuwa bado kufanya maaandalizi ya timu tulikuwa tunafanya mazoezi kila mtu kwake" alisema
pia aliongeza kulisema timu bado haiko vizuri kwakuwa ushindi tulioupata haiendani na kiwango cha wachezaji tuliocheza nao wachezaji wetu bado hawajaingia kambini na anawaheshimu wapinzani wao na mwalimu ameona makosa ya mchezo wa leo kwakuwa wanajiamini wataweza kufanya vizuri zaidi.
Mchezo wa Kesho polisi Vs New generation
Post a Comment