Zaidi
ya watu mianne wa kijiji cha Themiyasimba wilaya ya Arumeru
wameandamana hadi kwenye shamba la mwekezaji wakitaka kugawana sehemu ya
shamba ilo kwa madai mwekezaji amepewa shamba la hekari elfu tatu
lakini ameshindwa kuliendeleza na kuanza kuuuza kwa wawekezaji kutoka
nje huku wananchi wakikosa ardhi ya kuweka huduma muhimu za kijamii hali
iliyowalazimu viongozi wa kijiji na kata kuingilia kati kisha wananchi
wakatoa wiki moja la sivyo watafanya maamuzi magumu.
katika kijiji cha Themiyasimba na kulikuwa na umati mkubwa
wa wananchi waliyo zungumza kwa jazba wakisema wamefikia hatua hiyo
baada ya kuteseka kwa muda mrefu bila huduma za kijamii kama shule
zahanati na kituo cha polisi huku wakizungukwa na mashamba makubwa
yasiyo endelezwa na kuuzwa kwa wawekezaji kutoka nje ambao wengine
uyauza tena na kuwakata wananchi wanunue hekari moja kwa shilingi
milioni mbili huku wakitambua kwamba hawana uwezo huo.
Mwenyekiti wa kijiji cha Themiyasimba Emanuel Wiliam alitumia muda
mrefu kuwaomba wananchi kuacha kugawana shamba ilo kwakuwa ni kinyume
cha sheria na kuwataka kuwa nasubira wakati wakifanya mawasiliano na
uongozi wa juu.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Bwawani Lazaro Lukumay amesema
kumekuwa na tabia ya wawekezaji kupewa mashamba makubwa na kushindwa
kuyaendeleza kisha kuyauza na kuwakodisha wananchi kwa bei ya juu hivyo
ameitaka serikali kuangalia upya umiliki wake ili kuepusha migogoro
isiyo na tija.
Post a Comment