Rais
Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mwenyekiti wa Umoja wa
Afrika Dkt. Nkosazana Dlamini Zuma mara tu baada ya kuteuliwa kuwa
mwakilishi wa Afrika katika mchakato wa usuluhishi wa mgogoro wa Libya.
Mwenyekiti
wa Umoja wa Afrika Dkt. Nkosazana Dlamini Zuma amemteua Rais Mstaafu
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Mwakilishi wa Umoja wa Afrika katika
mchakato wa usuluhishi wa mgogoro wa Libya. Rais Mstaafu Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete ameteuliwa na Mheshimiwa Dkt. Nkosazana Dlamini Zuma,
Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (kulia) kuwa Mwakilishi wa
Umoja wa Afrika katika mchakato wa usuluhishi wa mgogoro wa Libya.
Kufuatia
uteuzi huo uliotangazwa rasmi na AU jana katika Kikao cha Wakuu wa Nchi
za Afrika, Rais Mstaafu Kikwete leo asubuhi amekutana na Dkt. Zuma makao
makuu ya AU leo na kufanya nae mazungumzo kuhusu jukumu alilokabidhiwa.
Mheshimiwa
Dkt. Kikwete amemshukuru Dkt. Zuma na Wakuu wa Nchi za AU kwa imani
kubwa waliyoonyesha kwake kwa kukabidhiwa jukumu hilo zito.
Amewashukuru pia wadau wa siasa nchini Libya kwa kuridhia uteuzi wake.
Naye Dkt.
Zuma amemshukuru Dkt. Kikwete kwa kukubali uteuzi huo na kuwa tayari
kubeba jukumu hilo. Amemueleza kuwa Umoja wa Afrika na Afrika nzima
inayo matarajio makubwa juu yake na iko nyuma yake. Amemuhakikishia
kumpa kila aina ya ushirikiano atakaouhitaji kukamilisha katika
kutekeleza majukumu yake.

Post a Comment