Rais Yoweri Museveni amezindua basi la kwanza katika eneo la Afrika mashariki linalotumia nguvu za jua.
Mabasi hayo yalitengezwa nchini Uganda na kampuni ya magari ya Kiira Motors Kayoola.Yalionyesha mara ya kwanza hadharani katika uwanja wa taifa Kampala mapema mwezi huu.
Moja ya betri zake inaweza kutiwa chaji na vibamba vyenye chaji ya miale ya jua vilivyopo katika paa la magari hayo ambavyo huongeza kasi ya gari hilo kufikia kilomita 80.
Iwapo yatatengezwa kwa wingi, kila basi linaweza kugharimu dola 58,000 ambayo bwana Musaizi anasema ni bei nzuri katika soko.
Post a Comment