0
 
Rais wa Misri Abdel Fattah el -Sisi
Serikali ya Misri, imeamuru kufungwa kwa kituo cha mwisho kilichobaki kwa ajili ya kuwatibu waathirika mateso.
Kituo cha El Nadeem kimeorodhesha ukiukaji wa haki za binadamu na kutoa ushauri nasaha kwa waathirika hao tangu mwaka 1993, lakini kituo hicho kimepewa mpaka wiki ijayo kufungwa.
Mamlaka ya nchi hiyo imesema imekiuka sheria za wizara ya afya.Mkuu wa kituo hicho, Aida Seif Al Dawla ameiambia BBC hatua hiyo ina mkono wa kisiasa.
Wiki mbili zilizopita, mwili ulionyofolewa viungo wa mwanafunzi wa kitaliano ulipatikana pembezoni mwa barabara, huku kukiwa na tuhuma kwamba alitekwa na vikosi vya usalama vya nchi hiyo, tuhuma ambazo Cairo imezikana.
Waziri wa mambo ya ndani wa Italy, amesema uchunguzi uliofanywa wa mwili huo umeonyesha alama za kushangaza zinazoashiria mateso aliyopitia mwanafunzi huyo.Uchunguzi wa kifo chake bado unaendelea.

Post a Comment

 
Top