Kijiko
cha Kampuni ya Udalali ya Mem Auctioneers and General Brokers Ltd
kikibomoa nyumba za makazi ya watu na biashara zilizojengwa katika eneo
la Kampuni ya Dar es Salaam Cold Makers Ltd lililopo Shekilango Sinza
jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
Kijiko kikibomowa moja ya baa zilizokuwepo eneo hilo jirani na Baa ya Rego iliyopo Sinza jijini Dar.
Wananchi, wamiliki wa nyumba na mabaa katika eneo wakiwa wamepigwa butwaa
Mabati yakiondolewa eneo hilo.
Hapa ni kupiga picha eneo la tukio na huzuni tupu.
Wananchi wakiwa eneo la tukio.
Kijiko kikibomoa nyumba ya ghorofa katika eneo hilo.
Askari Polisi na mgambo wakiwa eneo la tukio kuimarisha ulinzi.
Kontena
likiondolewa katika eneo hilo inadaiwa mmiliki wa kontenta hilo
aliuziwa eneo hilo miezi ya hivi karibuni kwa sh.milioni 400. hakika ni
hasara kubwa.
…………………………………………………………………………………………
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI
ya Udalali ya Mem Auctioneers and General Brokers Ltd imebomoa nyumba
za makazi ya watu na biashara zilizojengwa katika eneo la Kampuni ya Dar
es Salaam Cold Makers Ltd lililopo Shekilango Zinza jijini Dar es
Salaam.
Uvunjaji
wa nyumba hizo uliofanyika Dar es Salaam leo ambao ulisimamiwa na jeshi
la polisi na mgambo uliwaanja mdomo wazi na wasijue cha kufanya
wamiliki wa nyumba hizo na wafanyabiashara wa nyama choma ya nguruwe
ambao wengi wao walishindwa kuondoa mali zao na kujikuta wakiingia
hasara kubwa.
Akizungumza
na wanahabari eneo la tukio Meneja wa Biashara wa kampuni hiyo ya
udalali, Elieza Mbwambo alisema wamebomoa nyumba hilo kwa agizo la
mahakama baada ya mteja wao Dar es Salaam Cold Makers kushinda kesi ya
msingi iliyofunguliwa na mtu aliyetajwa kwa jina la Ondolo Chacha
aliyekuwa akidai eneo hilo ni lake.
Mbwambo
alisema kuwa eneo hilo lililokuwa linadaiwa kuwa ni mali ya Jumuiya ya
Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kampuni hiyo lilikuwa na mgogoro
tangu mwaka 1993 kati ya wamiliki halali na wavamizi ambayo ilikuwa
ikisikilizwa kwa nyakati tofauti ambapo mmiliki wake halali alikuwa
akishinda lakini watu wanaodaiwa wavamizi wakawa wanaweka pingamizi hadi
aliposhinda tena hivi karibuni.
“Baada
ya mmiliki halali kushinda kesi hiyo mahakama ilitupa kibali cha
kuwaondoa wavamizi ambao tumekuja kwaondoa baada ya kuwapa notisi lakini
mfungua kesi hakuweza kuwapa notisi hiyo jambo lililoleta changamoto ya
kwa watu waliokuwa wakitumia eneo hilo kushindwa kuokoa vitu vyao”
alisema Mbwambo.
Mbwambo
alisema mteja wao kwa zaidi ya miaka 20 alishindwa kutumia eneo hilo
kwa shughuli zake za uzalishaji mali kutokana na mgogoro.
Mmoja
wa wafanyabiashara katika eneo hilo aliyejitambulisha kwa jina moja la
James alisema yeye alipangishwa katika eneo hilo kwa kulipa sh.milioni
20 hivyo ameingia hasara kubwa ya ujenzi wa mabanda na vitu
vilivyokuwemo ambapo amepoteza zaidi ya sh.milioni 70.
Mfanyabiashara
huyo alisema eneo hilo walikuwa wakipangishwa na watu waliouziwa na mtu
aliyedai ni lake na miezi michache iliyopita kuna mzee mmoja aliuziwa
sehemu ya barabara na kutoa sh.milioni 400 na kujikuta akiingia katika
hasara kubwa.
“Tuta watafuta waliotuuzia maeneo katika eneo hilo na kutupangisha ili waweze kuturudishia fedha zetu” alisema James.
Post a Comment