Pep Guardiola
Mkufunzi wa timu ya
Bayern Pep Guardiola amesema hatua yake ya kuelekea katika kilabu ya
Manchester City haitaathiri kazi yake katika kilabu ya Bayern Munich
msimu huu.
Guardiola mwenye umri wa miaka 45,amekubali mkataba wa
miaka mitatu wa kuchukua mahala pake Manuel Pellegrini mwishoni mwa
msimu huu.Katika misimu misita ,kocha huyo wa zamani wa Barcelona ameshinda mataji 19 ikiwemo vikombe sita vya ligi na viwili vya bara Ulaya.
''Kwa nini vigumu?Mimi ni kama mwanamke,naweza kufanya kazi mbili mara moja na kudhibiti hali zote mbili.Nina talanta kubwa katika hili,''alisema Guardiola.
Guardiola ameripotiwa kukataa kandarasi mpya na kilabu hiyo ya Bundesliga mwaka uliopita na kutangaza mwezi Disemba kwamba ataondoka.
Post a Comment