Jamhuri ya Demokrasia ya Congo imefuzu kwa fainali ya mchuano wa CHAN.
Jamhuri ya Demokrasia ya Congo ilijikatia tikiti ya fainali baada ya kuilaza Guinea mabao 5-4 kwa mikwaju ya penalti.Mechi hiyo ilikuwa imeishia sare ya moja kwa moja katika muda waziada baada ya Ibrahim Sankhon kuisawazishia Guinea kunako dakika ya mwisho ya kipindi cha pili cha muda wa ziada.
Kimwaki,Mika,Jonathan Bolingi,Gikanji,Mechak Elia walifungia Leopards ya DRC huku
Ibrahim Sankhon,Leo Camara,Kile Bangoura,Daouda Camara wakiifungia Guinea.
Timu hizo zilitoshana nguvu muda wa kawaida na mechi ikaingia muda wa ziada uwanjani Amahoro, Rwanda.
Ni katika muda wa ziada ambapo Jonathan Bolingi Mpangi kunako dakika ya 101 alifanikiwa kutikisa wavu wa Guinea.
Mapema kwenye mechi, mchezaji wa DR Congo Padou Bompunga alipewa kadi ya njano dakika ya 38. Hili lina maana kwamba hataweza kucheza fainali iwapo timu yake itafuzu.
Rais wa Rwanda Paul Kagame ni miongoni mwa wageni mashuhuri waliohudhuria mechi hiyo.
DRC sasa watasubiri hadi kesho kujua mpinzani wao kati ya Mali na Cote de Voire.
Mechi hiyo ya nusu fainali ya pili imeratibiwa kusakatwa katika uwanja wa taifa wa Kigali kuanzia saa kumi jioni saa za Afrika ya kati.
- Ley Matampi
- Joyce Lomalisa
- Padou Bompunga
- Mechak Elia
- Doxa Gikanji
- Christian Ngudikama
- Nelson Munganga
- Merveille Bope
- Joel Kimwaki (Nahodha)
- Jonathan Bolingi Mpangi
- Yannick Bangala
- Abdoul Aziz Keita (nahodha)
- Mohamed Thiam
- Ibrahima Sory Bangoura
- Alseny Bangoura
- Ibrahim Sory Sankhon
- Ibrahima Sory Soumah
- Moussa Diawara
- Jean Mouste
- Alseny Camara
- Mohamed Youla
- Aboubacar Leo Camara
Post a Comment