
Leo Jumatano kulikuwa na mchezo,mchezo uliochezwa katika uwanja wa wilaya ya Liwale ilikuwa zamu ya timu ya Polisi Vs Mikukuyumbu World Soccer Mchezo uliokuwa wa aina yake kwani katika kipindi cha kwanza timu ya Polisi ilikuwa ya kwanza kupata goli namo dakika ya 32 na kupelekea kudumu goli hilo mpaka mapumzi.

Katika kipindi cha pili dakika chache waliongeza bao la pili na kupelekea timu ya Mikukuyumbu world soccer kubadili mchezo ili kuweza kusawazisha huku polisi ikiwakingia kifua ikitaka nayo kutoka na ushindi lakini namo dakika ya 69 Mikukuyumbu ilijipatia bao la kufutia machozi kwani Mikukuyumbu moja ya timu itayoshiriki mashindano ya ligi daraja ya tatu inayotarajia kuanza kutimua vumbi mwezi huu february.
Mpaka mpira unakamilika dakika 90 matokeo yalikuwa polisi 2 na Mikukuyumbu 1,Liwale Blog & Pride fm iliongea na nahodha wa timu ya Mikukuyumbu Shabani Mbwani a.k.a Bocho lii ili kuelezea juu ya mchezo.
"mchezo alikuwa si mbaya sana tupo kwenye mandalizi ya ligi na timu haijampata kocha mpaka sasa ila kocha anatalajiwa kupatika ndani ya siku zijazo kikubwa timu tufanye mazoezi pamoja na mashabiki wasikate tamaa timu itakuwa imara"alisema
kesho bonanza itaendelea tena kwa mchezo kati ya LIWALE UNITED Vs TRANSPORTER mchezo utakaochezwa kwenye uwanja wa wilaya mchezo utakao kuwa wa aina yake kwani Liwale united ilifungwa bao 4 kwa 1 dhidi ya Mikukuyumbu siku ya ufunguzi februari 1 na Transporter pia ilifungwa goli 2 bila dhidi ya Vijana star februari 2
Post a Comment