Aliyekuwa rais wa
shirikisho la soka duniani FIFA Sepp Blatter amesisitiza kuwa kura ya
kuandaa kombe la dunia mwaka 2022 haikupangwa ,akisema ''huwezi kununua
kombe la dunia''.
Blatter alisema kwamba hana hatia kufuatia madai
ya ufisadi huku akingoja uamuzi wa rufaa yake aliyoikata dhidi ya
marufuku ya miaka nane aliyopigwa na FIFA.Nina hakika kutakuwa na uamuzi wa haki na kwamba sijafanya uhalifu wa aina yoyote. Alisema Blatter.
FIFA ltamchagua rais wake mpya mnamo tarehe 26 mwezi Februari
Blatter alishinda kiti hicho kwa mara ya tano mnamo mwezi Mei lakini akapigwa marufuku kwa miaka minane kwa kumlipa pauni milioni 1.3 rais wa UEFA aliyesimamishwa kazi Michel Platini,malipo yanayodaiwa kuwa na utata.
Post a Comment