0
Mananasi ni matunda maarufu sehemu mbalimbali duniani. Ni matunda matamu yenye virutubisho vingi na muhimu kwa ufanyaji kazi bora wa mwili.

Mananasi ni chanzo kizuri cha kambakamba (dietary fibers), vitamini C na madini ya manganizi. Hayana fati wala lehemu (cholesterol). Mananasi yenye Vitamini C kwa wingi husaidia kuzuia utengenezwaji wa sumu za mwili (free radicals).Mananasi mabichi sio mazuri kiafya. Yanaweza yakakusabishia kuharisha, kutapika na maumivu makali ya tumbo

Virutubisho vilivyo ndani ya mananasi
Mananasi ni matunda matamu yenye sukari, vitamini C na madini ya manganizi kwa wingi. Mananasi hayana fati wala lehemu (cholesterol), na madini ya sodiamu kidogo.

Gramu 100 za nanasi zina virutubisho vifuatavyo;
Wanga gramu 13.2
Sukari gramu 10

Kambakamba gramu 1.4
Protini gramu 1
Fati gramu 0
Lehemu gramu 0
Vitamini C miligramu 47.8
Vitamini A

Madini ya Manganizi 0.978
Madini ya Kalsiamu miligramu 13
Madini ya Chuma miligramu 0.29
Mananasi yana kampaundi ziitwazo bromelain ambazo zinafanyiwa utafiti katika kusaidia katika maumivu ya viungo, kupunguza ukuaji wa vivimbe na kusaidia mmeng’enyo wa chakula.

Faida za Mananasi Kiafya

Huimarisha kinga ya mwili
Mananasi yana Vitamini C kwa wingi ambayo ni sehemu muhimu sana ya ufanyaji kazi wa kinga ya mwili. Huimarisha kinga na kuukinga mwili dhidi ya vijidudu mbalimbali.

Kuulinda mwili dhidi ya sumu za mwili (free radicals)
Sumu zinazotengenezwa na seli za mwili hushambulia na kudhuru seli za kawaida za mwili. Mananasi yana vitamini C ambayo husaidia kuondoa sumu hizi na hivyo kulinda seli za mwili.

Husaidia mmeng’enyo wa chakula kwenda vizuri
Mananasi yana kampaundi ziitwazo bromelain ambazo huwa na vimeng’enya vya protini. Vimeng’enya hivi hufanya chakula kisagwe na kunyonywa vizuri. Pia kambakamba na maji yaliyo kwenye nanasi husaidia kulainisha chakula kwenye utumbo na hivyo kuzuia choo kigumu au kukosa choo kwa muda mrefu.

Hupunguza hatari ya kupata pumu
Mananasi yana aina ya virutubisho vya beta-carotene, ambavyo pia hupatikana katika maembe, mapapai na karoti, ambavyo husaidia kupunguza uwezekano wa kupata tatizo la pumu.

Hupunguza hatari ya kupata saratani
Mananasi yana vitamini C, kambakamba na carotene ambazo husaidia kupunguza uwezekano wa kupata saratani. Vitamini C huondoa sumu za mwili (free radicals) ambazo huchangia kutokea kwa saratani, beta-carotene hulinda seli za tezi dume zisipate saratani na kambakamba ambazo hupunguza hatari ya saratani ya utumbo.

Kampaundi ya bromelain inayopatikana katika mananasi pekee husaidia kupunguza ukali wa madhara ya matibabu ya mionzi.

Kuboresha Uzazi
Vyakula vyenye madini na vitamini kwa wingi kama mananasi husaidia kuondoa sumu mwilini ambazo pia huathiri mfumo wa uzazi kwa wanawake na wanaume. Pamoja na matunda na vyakula vya majani vingine, inashauriwa kupata mananasi ili kuwa na ufanyaji kazi mzuri wa mfumo wa uzazi hasa kama unategemea kupata mtoto.

Ufanyaji kazi wa moyo
Mananasi yana madini ya potasiamu kwa wingi ambayo husaidia ufanyaji kazi mzuri wa moyo. Hupunguza hatari ya kupata shambulio la moyo na kiharusi.

Afya ya Ngozi
Ngozi hulinda mwili dhidi ya vijidudu, jua na kemikali mbalimbali ambavyo mwisho wa siku huichakaza ngozi. Vitamini C iliyopo kwenye mananasi huimarisha afya ya ngozi na kuifanya iwe laini, kung’aa na yenye afya.

Huimarisha mifupa
Kuongeza mananasi katika mlo wako

Unaweza kupata mananasi katika mlo wako kwa;

  • Kutengeneza mchanganyiko wa matunda, fruits salad, ikiwemo mananasi na matunda mengine.
  • Kupika mananasi na vyakula vingine kama samaki, kuku, nyama au kaa.
  • Kula vipande vya nanasi baada ya mlo
  • Tengeneza juisi yako ya nanasi, unaweza ukachanganya na matunda mengine.

Tahadhari
Kama una matatizo ya figo, ni vizuri ukatumia kiasi kidogo sana cha mananasi kwani figo haziwezi kuondoa kiasi kinachozidi.
Kama unatumia dawa za kundi la beta blockers, kula mananasi kwa kiasi.

Post a Comment

 
Top