Chelsea na West Brom watozwa faini
Mabingwa watetezi
wa ligi kuu ya Uingereza, Chelsea na West Brom wametozwa faini kwa utovu
wa nidhamu uwanjani katika mechi iliyozongwa na ubishi mwezi uliopita.
Shirikisho la soka nchini Uingereza FA limeitoza Chelsea faini ya pauni £65,000.West Brom kwa upande wake imepigwa faiani ya pauni £35,000.
Mhispania huyo alishambuliana na kiungo cha kati wa West Brom, Claudio Yacob baada ya kuangushwa.
West Brom walijifurukuta kutoka nyuma na kutoka sare na wenyeji wao Stamford Bridge.
Yacob, ambaye alikuwa keshaoneshwa kadi ya njano kwa kumuangusha Costa, aliondolewa uwanjani na kocha Tony Pulis.
Siku chache baadaye kocha wa muda wa Chelsea Guus Hiddink alielezea kutoridhika na uamuzi wa refarii Anthony Taylor, akisema kuwa alipaswa kumuonesha kadi nyekundu Yacob.
Post a Comment