WAMILIKI
wote waliokabidhiwa viwanda vya serikali baada ya kubinafsishwa, lakini
wakashindwa kuviendeleza, wametakiwa kuanzia Julai wawe wameanza
uzalishaji.
Vinginevyo, wameelezwa kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Waziri
wa Viwanda, Biashara ya Uwekezaji, Charles Mwijage alitoa tamko hilo
juzi mjini hapa baada ya kutembelea na kukagua viwanda vya serikali,
vilivyobinafsishwa kwa wawekezaji .
Mwijage
alimwagiza Mkurugenzi wa Viwanda wa wizara yake kufuatilia Wizara ya
Fedha na Mipango na taratibu mbalimbali za kisheria kwa wamiliki wa
viwanda, vilivyofungwa ama kushindwa kuendelea kuzalisha, kabla ya hatua
nyingine za kisheria kuchukuliwa kwa watakaoshindwa kutekeleza agizo .
“Viwanda
vya mashirika yote ambayo yalibinafsishwa na kupewa wawekezaji,
nahitaji kuona vinafanya kazi mwaka ujao wa bajeti Julai 2016,” alisema
Mwijage akiwa na Menejimeti ya Kiwanda cha Abood Seed Oil (Moproco).
Alisema
lengo la serikali ni kuona viwanda vyote vilivyobinafsishwa na
kushindwa kutimiza malengo yaliyokusudiwa, vinafanya kazi za uzalishaji
kulingana na maelekezo yaliyomo ndani ya mikataba ili kuwezesha kutoa
ajira nyingi za Watanzania.
Alisema
mkoa wa Morogoro ni wa uwekezaji wa viwanda na baadhi vilijengwa
kutokana na upatikanaji rahisi wa malighafi, zinatokana na sekta ya
kilimo .
Vile
vile alisema mpango wa ubinafsishaji, ulikuwa ni kutoa fursa pana kwa
wawekezaji kutoa ajira nyingi na kuongeza kasi ya uzalishaji wa bidhaa
kukuza uchumi, tofauti na ilivyo sasa.
“
Serikali ya awamu ya tano ni ya viwanda na Morogoro ni sehemu iliyopewa
kipaumbele cha kwanza cha uwekezaji wa viwanda vipya na kufufuliwa vya
zamani, hivyo ni jukumu la wizara yangu kuona viwanda vyote vinafanya
kazi kuanzia mwaka ujao wa fedha,” alisema akiwa na viongozi wa serikali
mkoani hapa.
Akiwa
katika kiwanda cha G&T Shoe ( Moro Shoe Ltd), Waziri alimwagiza
Mkurugenzi wa Viwanda wa Wizara, Obadia Nyagilo kuwasiliana na Mamlaka
ya Maeneo Huru ya Uuzaji Bidhaa Nje ya Nchi (EPZA), eneo hilo apewe
mwekezaji mwingine mwenye uwezo wa kujenga kiwanda .
Moro
Shoe Ltd ambacho kinamilikiwa na Guled Shoe Co. Ltd, kiliungua moto
kikiwa chini ya mwekezaji huyo na eneo hilo limebaki gofu. Waziri pia
aliagiza uangaliwe utaratibu wa namna ya kutwaa kiwanda cha Morogoro
Ceramic Wares Ltd na kupatiwa mwekezaji mwingine.
Kiwanda hicho kilichobinafsishwa kwa mwekezaji Pure Bond Ltd, kimefungwa kwa muda mrefu.
Waziri
alitaka apewe mwingine mwenye uwezo wa kuendesha uzalishaji wa bidhaa
aina nyingine zinazotumia malighafi za ndani. Alisema viwanda vilivyopo
Morogoro vinaweza kutoa ajira nyingi kwa wananchi wa Morogoro na nje ya
mkoa.
Awali,
Mkurugenzi wa Kampuni za Abood, Talal Abood, akitoa maelezo mafupi kwa
waziri huyo baada ya kutembelea kiwanda chao cha Morogoro Canvas Mill
(1998), ambacho kimefungwa, alisema hakifanyi kazi kutokana na
changamoto mbalimbali.
|
Post a Comment