0

Vurugu kubwa imetokea katika kikao cha kwanza cha kuapisha madiwani na kuchagua mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero baada mwenyekiti wa kikao hicho Yahya Nania kumtaka mbunge wa Kilombero Peter Lijualikali kutoka nje kwa kile kilicho daiwa kuwa sio mjumbe halali wa baraza hilo.
ITV imeshughudia jeshi la polisi likimtoa kwanguvu mbunge wa jimbo la Kilombero baada ya kuamuriwa na mwenyekiti wa kikao Bw. Yahya Nania kwa madai ya kwamba Simjumbe halali wa kikao hicho ambapo mvutano mkubwa ulitokea na mambo yalikua hivi.
 
Akizungumza baada ya mwenyekiti kutoa agizo la kutolewa mbunge huyo mbunge wa jimbo la Mlimba Suzan kiwanga amesema hakuna sheria inayoruhusu kumzalilisha kiongozi huyo kwa kumtoa kwa nguvu kwakuwa ni mjumbe halali wa kikao hicho na alichaguliwa na wananchi wa Kilombero kuwa mbunge wao. 
 
Naye mbunge wa jimbo la Kilombero Peter Lijualikali akizungumza mara baada ya kutolewa nje amelaani kitende hicho alichofanyiwa ambapo ameitaka serikali kuingilia kati swala hilo na kwamba swala hilo lisipofanyiwa ufumbuzi ataenda mahakamani ili haki itendeke huku mjumbe wa kanda Chadema Methew Likwina akiomba serikali kuingilia kati swala hilo vinginevyo kuwepo na uchaguzi mwingine wa mji mdogo wa Ifakara kuwa jimbo.
 
Vurugu hizo zilisababisha mwenyekiti wa kikao kuahirisha kikao kwa saa mbili na wajumbe walivyo rudi kwa mara ya pili hapakuwa na chakuongea ambapo aliahirisha kikao hadi kitakapo tangazwa tena.

Post a Comment

 
Top