Meneja
Habari Elimu na Mawasiliano wa Bodi ya Mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya
Juu Bw.Omega Ngole akiwaeleza waandishi wa Habari leo Jijini Dar es
salaam kuhusu utolewaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2014/2015 jumla ya
wanafunzi 99,069 walipata mikopo ambapo jumla ya bilioni 341
zimetolewa.kulia ni Mkurugenzi upangaji na utoaji mikopo Bw.Onesmus
Laizer.
Mkurugenzi
Upangaji na utoaji wa Mikopo toka Bodi ya Mikopo kwa wanafunzi wa
Elimu ya Juu Bw.Onesmus Laizer akitoa wito kwa wale wote walionufaika na
mikopo kurejesha ili kupanua wigo wautoaji mikopo hiyo na kuendana na
kasi ya serikali ya awamu ya tano.
…………………………………………………………………………………………………..
Frank-Mvungi-Maelezo
Serikali
imetumia bilioni 459 kuwakopesha wanafunzi wa elimu ya juu katika
kipindi cha mwaka 2015/2016 ambapo jumla ya wanafunzi 122,486
wamenufaika..
Hayo
yamesemwa na Meneja wa Habari Elimu na Mawasiliano wa Bodi ya Mikopo
kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu Bw. Omega Ngole wakati wa mkutano na
waandishi wa Habari leo Jijini Dar es salaam.
“Walionufaika
na mikopo katika kipindi cha 2015/2016 ni wengi na haijwahi kutokea
katika Historia tangu kuanzishwa kwa Bodi na haya ni matokeo ya
utendaji mzuri wa Serikali ya awamu ya tano “alisisitiza Ngole
Akizungumzia
utolewaji wa mikopo Katika kipindi cha mwaka 2014/2015 Ngole
alibainisha kuwa jumla ya wanafunzi 99,069 walipata mikopo na jumla
bilioni 341 zilitolewa .
Pia
Ngole alibainisha kuwa Serikali imeongeza idadi ya wanaufaika wa mikopo
kwa kuzingatia vipaumbele vinavyotokana na mahitaji ya Taifa.
Ngole amebainisha kuwa mafanikio hayo ni matokeo ya utekelezaji wa Falsafa ya Serikali ya awamu ya nne inayosema Hapa Kazi tu.
Aliongeza
kuwa Bodi hiyo inaendelea kufanya kazi kwa kuzingatia kasi ya Serikali
ya awamu ya tano itakayowezesha kutoa mikopo kwa wakati kwa kuzingatia
sheria Kanuni. na Taratibu za utoaji mikopo.
Bodi
ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya juu ni Taasisi ya Serikali
iliyoanzishwa kwa mujibu wa sheria Na.9 ya mwaka 2004 na kuanza rasmi
mwezi julai, 2005.ambapo Katika mwaka wa Masomo 2005/2006 idadi ya
wanafunzi waliopata mikopo ilikuwa 42,749 ambapo jumla ya bilioni 56.1
zilitolewa
Post a Comment