0

Diwani wa kata ya Igombavanu iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa Mh. HABIBU KILONGE amefariki Dunia katika hospitali ya wilaya ya Mufindi usiku wa kuamkia leo ilikokuwa amelazwa kwa matibabu.
Taarifa ya mwenyekiti wa Halmsahauri ya Wilaya ya Mufindi Mh. FESTO MGINA kupitia kitengo cha habari na mawasiliano cha Halmashauri ya Wilaya, ameeleza kuwa, marehemu amefarikia baada ya kusumbuliwa na maradhi kwa takribani mwezi mmoja na mara kadhaa alikuwa akitibiwa katika hospitali ya Wilaya na kurejea nyumbani.
Aidha, amebainisha ratiba ya shughuli za maziko kuwa marehemu atazikwa Jumapili ya Tarehe 17 ambapo mapema asubuhi ya saa mbili mwili wa marehemu utaondolewa katika Hospitali ya Wilaya Mafinga na kupekwa katika kata ya Igombavanu ambakoa utaagwa na wapiga kura wake na itakapofika saa tano asubuhi mwili huo utasafirishwa kwenda Kijiji cha kichiwa Mtwango Mkoani Njombe ambako ndiko mwili huo utazikwa.
Marehemu Diwani HABIBU KILONGE alichaguliwa kwa mara ya kwanza na wananchi wa Kata ya Igombavanu kupiti atiketi ya chama cha Mapinduzi CCM katika uchaguzi Mkuu uliyofanyika mapema mwezi wa 10 mwaka jana kwa jumla ya kura Elfu 2 na 34 ikiwa ni ushindi mkubwa dhidi ya mpinzani wake wa karibu kutoka chama cha Chadema aliyepata kura 361 na mpaka mauti inakuta diwani huyo alikuwa amehudhuria kikao kimoja pekee, ambacho kilikuwa maalu kwa kuapishwa.

Post a Comment

 
Top