0


Mbunge wa Jimbo la Liwale,Zuberi Kuchauka akifuatilia kwa ukaribu matengenezo ya X-ray katika Hospitali ya Wilaya ya Liwale.
 Fundi wa X-ray akiwa makini katika jitihada ya kuitengeza mashine hiyo ili wananchi wa jimbo la Liwale waweze kupata huduma karibu. 

Halmashauri ya wilaya Liwale imeanza  kufanyia matendengezo ya X-ray ambayo iliyosimama  kwa muda wa zaidi  miezi  tisa  na kupelekea wagongwa wanaohitaji vipimo vya x-ray kusafiri umbali  mrefu kufuata huduma hiyo.

Hayo yameelezwa na  mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Gaudence Nyamihula wakati alipokuwa anazungumza na timu ya waandishi wa habari waliotembelea wilayani humo.  

"Uongozi wa wilaya  ulifanyamawasiliano na  wizara ya afya  na kupatiwa fundi  kutoka  Kampuni ya Philips ambayo ndiyo yenye mkataba wa kufanya matengenezo ya mashine hizo.
 
Nyamihila  alisema mashine hiyo ilikuwa na tatizo la kufa betri  na itilafu zingine za kiufundi  lakini   kipindi  hiki mashine hiyo inatendenezwa ili wagonjwa wanaohitaji vipimo hivyo waweze kwenda kupatiwa huduma katika hospitalini hapo.
 
Kwa upande wake  Mganga mkuu  Dkt Maltin alisema Hospitali  ya wilaya inakabiliwa na changamoto  ikiwemo upungufu wa watumishi  damu salama, dawa, vifaa tiba, uchakavu wa majengo na eneo la kutenga watu wenye magonjwa ya kuambukiza ukiwemo Kipindupindu.
 
Alisema mbali ya upungufu huo, wapo baadhi ya watumishi hasa wauguzi ambao kuacha kazi muda mfupi baada ya kuajiriwa kutokana  mazingira ya kijiografia ya wilaya  na kuongeza upungufu zaidi.
 
Nae Mbunge  wa jimbo la Liwale, Zuberi kuchauka alisema tatizo la X-ray limekuwa kero kwa wananchi na wagonjwa katika wilaya hiyo  kutokana na kutumia  fedha  na muda mwingi kuangaikia huduma hiyo nje ya wilaya.

Post a Comment

 
Top