Waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako amefuta rasmi mfumo wa kukokotoa matokeo kwa mtindo wa GPA.
Ameagiza
matokeo ya kidato cha 4 na 6 yatolewe kwa mfumo wa madaraja (divisions)
kama ilivyokuwa hapo zamani.Maamuzi haya yanakuja baada ya waziri huyo
kuwapatia baraza la mitihani, wiki moja kuumpa sababu za kubadili mfumo
wa utunuku viwango vya ufaulu wa awali na kwenda kwa wastani wa pointi
(GPA) unaotumika sasa Kidato cha Nne na Sita.
Waziri
Ndalichaki amesema amefikia uamuzi huo baada ya Baraza la Mitihani
(NECTA) kushindwa kutoa utetezi wa kisayansi juu ya sababu zilizopelekea
wao kubadili mfumo wa upangaji madaraja ya ufaulu kwa wanafunzi
Mfumo wa
GPA ulianza kutumika kwa wanafunzi waliofanya mtihani wa mwaka 2014
ambao matokeo yao yalitoka mwaka jana. Mwaka 2013, ya asilimia 60 ya
wanafunzi wa kidato cha nne walifeli mitihani wa kitaifa, hali ilioleta
kwa matokeo hayo kurudiwa tena ili kuwafaulisha wanafunzi zaidi
|
Post a Comment