Chama cha Wananchi (CUF) kimesema hakitakubali marudio ya uchaguzi wa urais visiwani Zanzibar.
Chama hicho kupitia taarifa kwa wanahabari kimesema hakuna “hoja wala msingi wa kikatiba na kisheria wa uchaguzi kurudiwa”.Taarifa ya chama hicho ambayo imesomwa na mgombea wa urais wa CUF katika uchaguzi wa 25 Oktoba mwaka jana Maalim Seif pia inaonekana kupendekeza mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha ang’atuke.
Chama hicho kimemtuhumu Rais wa visiwani Mohamed Ali Shein wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kukwamisha mashauriano ya kutafuta suluhu ili ZEC itangaze marudio ya uchaguzi tarehe 28 Februari 2016.
CCM imeonekana kuunga mkono kurudiwa kwa uchaguzi visiwani na majuzi viongozi wa chama hicho waliwataka wafuasi wake visiwani kujiandaa kwa marudio ya uchaguzi.
Tangazo hilo lilishutumiwa vikali na viongozi wa CUF.
Post a Comment