0
                              
Chama cha Wananchi, CUF, kimemtaka Rais John Pombe Magufuli wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuingilia moja kwa moja na kuongoza mazungumzo ya kusaka suluhisho la mkwamo wa kisheria na kikatiba visiwani Zanzibar, kwani jitihada za kutafuta suluhu ya kisiasa zinazoendelea kufanyika baada ya kufutwa kwa uchaguzi wa Oktoba 25 zinatiwa walakini.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Hoteli ya Serana, jijini Dar es Salaam, hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa CUF ambaye ndiye aliyekuwa mgombea wa urais wa Zanzibar kwa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam mapema leo.

Post a Comment

 
Top