0

 Breaking News: Yanga yavunja mkataba na Niyonzima
Uamuzi huo umefikiwa na kikao cha Kamati ya Nidhamu ya klabu, baada ya kulichunguza kwa umakini suala la mchezaji huyo na historia yake ya nidhamu pia ndani ya klabu tangu asajili
Klabu ya Yanga imevunja Mkataba na kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Haruna Niyonzima kutokana na mchezaji huyo wa kukiuka vipengele vilivyopo kwenye mkataba wake, ikiwemo tatizo la utovu wa nidhamu.
Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha ameiambia Goal, leo wamevunja mkataba na nahodha huyo wa timu ya taifa ya Rwanda na pia tatakiwa kuilipa Yanga fidia za garama ilizotumia kwa ajili yake wakati wote tangu aliposaini mkataba mpya wa miaka miwili miezi mitano iliyopita.
Tiboroha amesema uamuzi huo umefikiwa na kikao cha Kamati ya Nidhamu ya klabu, baada ya kulichunguza kwa umakini suala la mchezaji huyo na historia yake ya nidhamu pia ndani ya klabu tangu asajiliwe miaka minne iliyopita.
Sakata la sasa la Niyonzima linaanzia mwezi uliopita baada ya mchezaji huyo kuruhusiwa kwenda kuichezea Rwanda katika Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki, CECAFA Challenge nchini Ethiopia na akachelewa kurejea baada ya mashindano.

Kufuatia hali hiyo, klabu ilimsimamisha kwa muda usiojulikana Niyonzima kabla ya suala lake kupelekwa Kamati ya Nidhamu, ambayo hatimaye imekuja na maamuzi magumu.
Pamoja na Niyonzima kuwasilisha vielelezo vyote vya kumsafisha, lakini uchunguzi wa Kamati ya Nidhamu ulijiaminisha kiungo huyo amedanganya ili kukwepa hatua za kinidhamu.

Ulibaini plasta gumu (PoP) alilofunga baada ya kurejea akiwa amechelewa ilikuwa ni ‘geresha’ na vielelezo vingine alivyowasilisha vilikuwa ‘feki’ pia.

Na ikamnasa kwenye picha za video siku za karibuni ‘akijirusha’ sehemu mbalimbali za starehe ikiwemo kwenye onyesho la mwanamuziki Ali Kiba.

Post a Comment

 
Top