Kampuni 43 ambazo
zinamiliki makontena 329 yaliyokamatwa bandarini Tanzania wakati wa
ziara ya kushtukiza ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa zimetambuliwa.
Kaimu kamishna mkuu wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) Dkt Philip Mpango amesema sasa zimesalia siku sita kwa kampuni hizo kulipa kodi inayotakikana.
Kampuni 4 tayari zimejitokeza na kulipa Sh5 bilioni.
Makonteina hayo yalikamatwa katika bandari kavu ya kampuni ya Said Salim Bakhresa.
Bidhaa zilizokuwemo ndani ya makontena hayo ni pamoja na matairi ya magari,vifaa vya ujenzi, betri za magari, nguo na bidhaa nyingine.
Watuhumiwa 8 wanaoshukiwa kuhusika katika kupitishwa kwa makontena hayo 329 wamefikishwa Mahakama ya Kisutu leo wakikabiliwa na makosa ya kuhujumu uchumi, kusababisha hasara ya Sh12.7bn.
Aidha, kufikia sasa, watumishi 35 wa TRA katika ngazi mbali mbali wamesimamishwa kazi wakiwemo 27 waliokamatwa katika ziara hiyo ya kushtukiza ya Bw Majaliwa.
Hayo yakijiri, watumishi wote wa TRA wametakiwa kuwasilisha taarifa sahihi ya orodha ya mali zao zote kwa ajili ya uhakiki wa kina kufikia tarehe 15 Desemba.
Post a Comment