Muungano unaoongozwa na Saudi Arabia unaopigana vita nchini Yemen
unasema kuwa usitishwaji mapigano wa siku saba na waasi wa kishia wa
Houthi umeanza kutekelezwa.
Usitishwaji huo unaenda sambamba na kuanza kwa mazungumzo ya amani yanayofadhiliwa na umoja wa mataifa yanayofanyika nchini Uswisi.
Mapigano yaliendela hadi dakika za mwisho za kuanza kwa usitishwaji huo huku vikosi vya serikali vinavyosaidiwa na mashambulizi ya angani ya Saudi Arabia vikiteka kisiwa kilichokuwa kikishikiliwa na waasi katika bahari ya shamu.
Watu 6000 wanaaminika kuuawa tangu Saudia Arabia iingilie kati mzozo nchini Yemen mwezi Machi.
Umoja wa mataifa umeiambia pande zote katika mazungumzo hayo kuwa mpango wa kuleta amani huhitaji ujasiri.
Agenda ya mkutano huo hata hivyo huenda ikawa ngumu kutekeleza.
Dhamira kuu ni kuhakikisha kuwepo kwa usitishwaji wa mapigano kabisa baada ya mkataba wa awali wa kusimamisha vita kwa muda kumalizika.
Aidha mpango wa kuondoa makundi yaliyojihami na silaha nzito nzito, kuruhusu mashirika ya kutoa misaada ya kibinadam katika maeneo yote na pia mpango wa kubadilishana wafungwa ni baadhi tu ya mambo yanayotarajia kujadiliwa.
Hata hivyo masuala hayo yote hayawezi kujadiliwa na kuidhinishwa kwa siku moja au mbili, lakini mabalozi hao wa umoja wa mataifa wanasema watachukua muda unaohitajika.
Haya yote yameashiria jinsi umoja wa mataifa umejitolea kuhakikisha kupatikana kwa mkataba.
Huku asilimia 8o % ya raia wakihitaji misaada ya kibinadam, Yemen haina lingine kwa sasa ila kupatikana na amani.

Post a Comment