Mapya yamezidi kuibuka katika sakata la ufisadi kwenye mkopo wa Sh1.3
trilioni kutoka Benki ya Standard baada ya asasi ya kiraia nchini
Uingereza kubainisha kuwa Serikali imepunjwa fidia katika uamuzi wa kesi
hiyo.
Katika sakata hilo, Serikali ilitaka mkopo wa Dola 600 milioni kupitia hati fungani na benki ya Stanbic ilitaka mgawo wa asilimia moja, sawa na Sh 13 bilioni, kwa njia ya kifisadi kufanikisha kupatikana kwa mkopo huo kampuni mama ya benki ya Standard ya Uingereza.
Ripoti ya uchambuzi ya asasi ya kiraia ya Corruption Watch ya Uingereza inaeleza namna suala hilo lilivyoendeshwa na upungufu wake ikisema Tanzania ilistahili kupata Dola 80 milioni (sawa na Sh170 bilioni) badala ya Dola 6 milioni (12.6 bilioni) kama fidia ya hasara iliyotokana na ufisadi huo.
Sakata hilo liliibuka mwishoni mwa Novemba baada ya Taasisi ya Uchunguzi wa Makosa Makubwa ya Ufisadi ya Uingereza (SFO) kutoa ushahidi wake katika Mahakama ya Southwark Crown ya jijini London, Uingereza jinsi ukiukwaji wa taratibu za kibenki ulivyosababisha Sh13 bilioni kuingizwa kifisadi kwenye kampuni ya Egma iliyokuwa ikijifanya ni wakala.
“Hata hivyo faida ambayo benki ilipata ambayo ilielezwa kuwa Dola 8.4 milioni za Marekani haikutilia maanani mtiririko wa mapato ambayo benki hiyo ilipata kutokana na muamala huo ambao huenda ungekuwa Dola 10 milioni, wala haikuangalia faida za kisoko ambazo benki ilipata kama sehemu ya uovu huo,” inasema ripoti hiyo.
Benki ya Standard ina hisa kwenye benki ya South African Group ya Afrika Kusini ambayo ndiyo inaimiliki Stanbic tawi la Tanzania. Kampuni mama ya benki hizo zote ni Industrial and Commercial Bank of China (ICBC) ambayo imekiri kushindwa kuzuia ufisadi huo.

Post a Comment