Akiongea mjini Bukoba afisa mfawidhi wa uvuvi mkoani Kagera
Apolinary Kyojo amaesema uvuvi haramu katika ziwa Victoria bado nitishio
kubwa kwakuwa wavuvi waliowengi hutumia zana haramu ambazo maranyingi
zimekuwa zikiteketeza samaki wachanga na kuhalibu mazalia ya samiki hali
ambayo inaweza kupelekea kutoweka wa samaki katika ziwa hilo.
Akizungumza mara baada ya kutekeza zana hizo haramu za uvuvi mkuu
wa mkoa wa Kagera John Mongella amesema serikali haikotayari kuwavumilia
wavuvi wanaokiuka sheria na kanuni za uvuvi kwa kutumiwa zana haramu
pamoja na madawa yenyesumu kali ambayo yamekuwa yakiathiri mazalia ya
samaki huku akiahidi kudhibiti vyanzo vya zana haramu ambazo maranyingi
zimekuwa kikwazo katika uvuvi wa samaki.
Nao baadhi ya maofisa wa doria katika ziwa Victoria wamesema pamoja
kukamata zana hizo haramu pia wamekuwa wakikabiliana na changamoto
mbalimbali katika opresheni zao ikiwemo wavuvi kubuni mbinu mpya ya
kuficha zana za uvuvi kwa kuzichimbia chini ya mchanga huku baadhi ya
wananchi wakilalalamikia kupanda kwa bei samaki kiholela kunakosabishwa
na tatizo la uvuvi haramu.
Post a Comment