Mkazi mmoja anayoitwa Yanini Saidi Liwango (35) wa kijiji cha
Lilombe A kata ya Lilombe wilayani Liwale mkoani Lindi amefariki leo asubuhi
baada ya kupigwa na kitu chenye ncha kali kwenye paja la kulia .
Tukio hilo limetokea jana usiku
majira ya saa 4 usiku maeneo ya kandokando ya mto Lilombe barabarani baada ya
watu waliokuwa wanasafiri waliokuwa wanatoka Tunduru kumuona akigagaa ndipo mwalipofika kijijini Lilombe A kwenye mkusanyiko
wa watu kutoa taarifa ambapo walipotoa taarifa hiyo ni kwenye Msiba wa baba
mdogo wa marehemu aliyefariki jana kwa
maradhi katika hospitali ya wilaya ya Liwale.
Kaka wa marehe Zuberi Saidi Liwango aliongea na mwandishi wa
Liwale blog alisema Yanini Liwango
(marehemu)baada ya kutokea kifo cha baba yao mdogo Athumani Liwango kilichotokea katika hospitali ya Liwale
na maiti ilisafirishwa mpaka kijijini kwao kwenye familia yao, Yanini (marehemu) ni miongoni
mwa wtu waliotumwa kwenda kutoa taarifa ya msiba wa baba yao mdogo kwa ndugu
wengine yeye alienda katika kijiji cha Kiegei ndipo alikutwa na mkasa huo.
Zuberi alisema baada ya kupata
taarifa iliyoletwa kutoka kwa wasafiri hao alikuwa na wasiwasi maana baadhi ya
ndugu wa familia hiyo walikuwa wametumwa maeneo mbalimbali kwa ajili ya kutoa
taarifa ya msiba aliamua kwenda na ndugu yake wakiwa na usafiri wa pikipiki
mpaka eneo la tukio walioambiwa usiku ndipo walipo muona alikuwa ndugu yao akiwa anajeraha
anavunjwa damu nyingi baada ya kupigwa na kitu chenye ncha kali huku akiwa amebakiwa na nguo ya ndani na baiskeli aliokuwa ameitumia kusafiria hawajaikuta baada ya
kuulizwa nini Yanini alisema neno moja kuwa AMEPIGWA RISASI
na kuzimia ndipo Zuberia alirudi mpaka kijijini
kutoa taarifa na kuchukua gari kumfuata mgonjwa maana kutokana na jeraha
walishindwa kumbeba kwenye pikipiki.
Baada ya kumfisha hospitali daktari
baada ya kumfanyia vipimo alikuwa Yanini amefariki ndipo familia ya marehemu waliambiwa marehemu anatakiwa
achunguzwe ili kujua tatizo
lililopelekea mapaka marehe apoteze uhai.
Mganga mkuu wa wilaya Martin Mwandiki
alipomfanyia uchunguzi wa kitaalamu mwili wa marehe akiwa na ndugu wa marehemu
Liwango Saidi Liwango na askari polisi mganga mkuu baada ya ufanya upasuaji
alikikuta kitu aina ya plastiki chenye mzunguko wa duara ndani ya paga la kulia
kwenye jeraha pia alisema marehe alivujwa damu nyingi,Familia ya marehemu
waliruhusiwa kuchukua maiti kwenda kuzika na kujikuta familia hiyo ya Liwango kuzika misiba miwili huko kijini kwao Lilombe A.
Katika tukio hili mkuu wa wilaya ya Liwale
mh,Ephraim Mmbaga na kamanda wa polisi wa wilaya Raphael Mwandu walifika
Hospitali ya wilaya na wamethibisha kutokea kwa tukio hili na walishauri ipo
haja ya ukamilishaji wa haraka wa kituo kidogo cha polisi katika kijiji hicho
cha Lilombe kwani kijiji hiko lilishaabiwa wajenge jingo la kituo kidogo mpaka
sasa ujenzi wake haujakamilika.
Post a Comment