REAL
MADRID wameondolewa kwenye michuano ya kombe la Copa Del Rey wiki
iliyopita na juzi wameendelea kufanya vibya kwenye ligi baada ya
kukubali kipigo cha 3 msimu huu mbele ya Villareal – jambo ambalo
limezidisha presha kwa kocha, Rafa Benitez.
Na Je inawezekana pia wakawa wanaelekea nje ya michuano ya ulaya pia? Historia inatoa ishara kwamba hiyo inaweza kutoka.
Wababe hawa wa kihispania walipangwa na AS Roma katika droo
iliyofanyika jana ya hatua ya 16 bora – Madrid hawajawahi kuitoa timu
yoyote ya Italia katika hatua ya mtoano katika kipindi cha miaka 29
iliyopita. Klabu
hiyo yenye mafanikio zaidi katika michuano ya barani ulaya wameondolewa
kwenye michuano hii na AC Milan, Torino, Juventus wakawatoa mara 4 na
hata AS Roma pia imewahi kuwaondoa kwenye michuano hii.
Mara ya mwisho kwa Madrid kuitoa timu ya italia kwenye michuano hii ya ulaya ilikuwa mwaka 1987 vs Napoli.
REKODI YA REAL MADRID VS TIMU ZA ITALIA
1988-89 European Cup semi-final
Real Madrid 1 AC Milan 1
AC Milan 5 Real Madrid 0 1989-90 Europen Cup second round
AC Milan 2 Real Madrid 0
Real Madrid 1 AC Milan 0 1991-92 Uefa Cup semi-final
Real Madrid 2 Torino 1
Torino 2 Real Madrid 0 1995-96 Champions League quarter-final
Real Madrid 1 Juventus 0
Juventus 2 Real Madrid 0 2002-03 Champions League semi-final
Real Madrid 2 Juventus 1
Juventus 3 Real Madrid 1 2004-05 Champions League last 16
Real Madrid 1 Juventus 0
Juventus 2 Real Madrid 0 (Aet) 2007-08 Champions League last 16
Roma 2 Real Madrid 1
Real Madrid 1 Roma 2 2014-15 Champions League semi-final
Juventus 2 Real Madrid 1
Real Madrid 1 Juventus 1 Pedrag
Mijatovic akiifungia Real Madrid goli la ushindi dhidi ya Juventus
katika fainali ya UCL 1998 – Hii ilikuwa mara ya kwanza kwa Madrid
kupata kuweza kuitoa au kushinda mechi ya hatua isiyo ya makundi dhidi
ya timu ya Kiitaliano tangu mwaka 1966
Hata hivyo Real Madrid walifanikiwa kuifunga Juventus kwenye fainali ya Champions League mwaka 1998.
Post a Comment