korosho waliokuwa wameziokota kutoka shamba lao la mikorosho
Philimon Kaspal Punda aliyekaa katikati akipewa msaada wa usafiri
Kijana mmoja anayefamika Limu Philimon Punda mwenye umri wa
miaka 18 amemua mama yake mzazi bi Christina Raymond Mposa mwenye umri wa miaka
41 kwa kumchoma kisu kwenye ziwa na kufaliki hapohapo na kumjeruhi baba yake
mzazi Philimon Kaspal Punda shambani kwao majira ya saa 3 usiku jana katika
kijiji cha Tepetepe kata ya Mungurumo wilayani Liwale mkoa wa Lindi.
Tukio hili la kikatili lilitokea katika shamba la mikorosho kwa wazazi wa Limu punda ambaye
aliyefanya ukatili huu wakiwa katika shughuli za kilimo za kuokota korosho
ghafla alikuja mtoto wao Limu Punda na kuanza kumshambulia baba yake Philimon
Punda na kumjeruhi usoni maeneo ya jicho la kushoto na mkononi karibu na begani
na baada ya kufanya tukio kijana huyo kutokomea kusikojulikana .
Mashaka Punda ambaye mtoto wa Philimon ambaye shuhuda wa tukio
alisema baada ya kaka mtu anamsha baba
yao ndipo mama yao kwa sasa marehemu alienda kuamua ugomvu ndipo alipochomwa
kisu kwenye ziwa na kufaliki hapohapo ndipo baba na watoto wake wawili kuelekea
kwa majirani kuomba msaada.
Philimon Punda yupo kwenye hospital ya wilaya ya Liwale akiwa
anapata matibu baada ya kuvujwa damu nyingi.
Katika tukio lingine Limu Punda majira ya saa moja karo usiku
alimjeruhi bi Hajra Ally Nyimage mkazi wa kijiji cha mungurumo kata ya Liwale
mjini ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari
ya Rashidi Mfaume Kawawa(R.M)
Hajra nyimage akiongea na mwandishi wa habari kwenye hospital
ya wilaya ya Liwale akiwa kwenye matibabu leo alisema kijana huyo leo siku ya pili kuja kujeruhi siku ya kwanza ilikuwa mwezi uliopita
arimjeruhi na jana alimjeruhi mkono wa kushoto sehemu mbili na mkono wa kulia
kwenye kidole na ameshonwa nyuzi sita.
Kamanda wa polisi wa wilaya ya Liwale Rapheal Mwandu amethibisha
kutokea kwa matukio haya mawili na jeshi lake linasaka Limu Punda aliyefanya
ukatili huo ili kumfikisha kwenye mkono wa sheria.



Post a Comment