Serikali ya Iraq
imeiamuru Uturuki iondoe wanajeshi wake katika eneo la mpakani karibu na
mji wa Mosul ambalo linadhibitiwa na wapiganaji wa Islamic State.
Mamia ya wanajeshi wa Uturuki, wakitumia vifaru, walivuka mpaka na kuingia eneo hilo, lengo lao likiripotiwa kuwa kuwapa mafunzo wapiganaji wa Kikurdi nchini Iraq ambao wamekuwa wakipambana na wapiganaji wa Islamic State.
Ripoti zinasema wanajeshi 150 walikuwa wametumwa katika mji wa Bashiqa.
Mji wa Mosul umekuwa ukidhibitiwa na wapiganaji wa Islamic State tangu mwaka jana na juhudi za Iraq kujaribu kuukomboa hazijafanikiwa.
Post a Comment