0
Chicharito 1
Mshambuliaji wa zamanin wa Manchester United Javier Hernandez anayetamba kwa sasa na klabu yake mpya ya Bayer Leverkusen ya Ujerumani ameibuka na kuvunja ukimya juu ya kuondoka kwake kwenye klabu ya Manchester United.
Chicharito ameandika waraka akielezea namna ambavyo kocha Lois van Gaal alifanya kila awezalo kuhakikisha nyota huyo anaondoka kwenye kikosi cha Man U.
Hapa Chicharito anaeleza namna alivyoondoka Manchester United na sababu zilizopelekea yeye kwenda Ujerumani na si kubaki England.
Baada ya kukosa mkwaju wa penati na kumuona akimpa Giggs maelekezo nikaanza kujua nimepoteza nafasi yangu kwenye timu.
Wakati tupo kwenye vyumba vya kubadilishia nguo alikuja kwangu na kuniambia; “kama umekosa penati ninamashaka kama unaweza kufunga goli katika hali ya kawaida.
Hayakuwa maneno mazuri kwangu, alinivunja moyo kwa kiasi kikubwa pale aliponiambia itanichukua miaka kadhaa kupata nafasi mbele ya James Wilson.
Baada ya siku moja aliniita ofisini kwake na kuniambia, kuna offer nyingi zipo mikononi mwake juu yangu na kuniambia natakiwa kuchagua timu ya kwenda.
Nilirudi nyumbani na kulia kwa mara ya tatu kama mchezaji niliyeipenda Manchester United. Nipenda kucheza Manchester United lakini lakini sikua na cha kufanya yeye alibaki kuwa mwamuzi wa mwisho.
Kulikuwa na offer mbili kutoka timu za America, tatu zilikuwa za EPL moja kati ya hizo ilikuwa ni Spurs, lakini nilipofikiria nikibaki England ntacheza dhidi ya Manchester United niliamua kuchagua kwenda Bayer Leverkusen.
Pia aliniambia kuwa sikua na-fit kwenye philosophy zake lakini mimi nadhani yeye ndio ha-fit kwenye philosophy yangu. Bado naendelea kuwasiliana na wachezaji wenzangu hasa wale ambao tulicheza pamoja chini ya Sir Alex Ferguson. David de Gea alikuwa ni rafikiangu mkubwa tulizungumza karibu kilasiku, Carrick pia, Ashley Young hata Rafael da Silva.
Nazungumza nao mambo binafsi kwa ujumla, lakini kitu pekee nachoweza kusema ni kwamba wachezaji senior hawana furaha.
Kama nikipewa nafasi napenda kucheza Machester United tena, lakini kwa sasa ninafuraha na ninafurahia maisha ya Ujerumani.
Javier Hernandez
Video ya Chicharito alivyopiga hat-trick kwenye mechi ya  Bayer Leverkusen vs Borussia Monchengladbach

Post a Comment

 
Top