Ajali ya pikipiki imemgonga mpanda baiskeli Mshamu Salum
Majura(80) na kusababisha kifo ajali hiyo imetokea leo decemba 29 majira ya saa
8 mchana katika kijiji cha Mbaya kata ya
Mbaya wilayani Liwale mkoani Lindi.
Mwendesha pikipiki na mkazi wa kijiji cha Mbaya Miraji Rajabu Kauka
(22) aliokuwa akiendesha pikipiki yenye namba T599DE aina ya SANLG alimgonga
Majura maeneo ya kichwani na mkono wa kushotona kufariki dunia.
Kamanda wa polisi wilaya ya Liwale Raphael Mwandu amethibitisha
kutokea kwa ajali hiyo na alisema mtuhumiwa amelazwa katika hospitali ya wilaya
ya Liwale na hali yake ni mbaya.

Post a Comment