Wachezaji
wa Uganda Cranes wakifurahia moja ya mabao waliyowafunga Zanzibar
Heroes katika michuano ya CECAFA inayofanyika nchini Ethiopia
UGANDA
imezinduka katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na
Kati, CECAFA Challenge baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya
Zanzibar jioni ya leo mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Huo
unakuwa mchezo wa pili mfululizo kwa Zanzibar Heroes kufungwa, baada ya
awali kugungwa 1-0 na Burundi na sasa inajiweka katika mazingira magumu
kwenda Robo Fainali.
Mabao ya Uganda katika mchezo huo wa
Kundi B yamefungwa na Farouk Miya dakika ya 10 na 18, Erisa Ssekisambu
dakika ya 48 na Ceasar Okhuti dakika ya 79.
Zanzibar
ilipoteza wachezaji wawili kwa kadi nyekundu katika mchezo huo, kwanza
kipa wake Mwadini Ally dakika ya 13 na baadaye kiungo Mudathir Yahya
dakika ya 74, wote wa Azam FC ya Dar es Salaam. Zanzibar itamaliza na
Kenya wakati Uganda itamaliza na Burundi.

Post a Comment