0
 
Mamlaka ya upangaji uzazi imesema ni lazima sheria ifanyiwe marekebisho kwanza
Mamlaka kuu inayosimamia upangaji wa uzazi nchini Uchina imeonya wanandoa nchini humo kwamba sharti waendelee kutii agizo la kuwa na mtoto mmoja kwenye familia hadi sheria ifanyiwe marekebisho mwezi Machi.
Alhamisi wiki jana, serikali ilitangaza kwamba ingelegeza sheria na kuwaruhusu wanandoa kuzaa watoto wawili.
Ilisema uamuzi huo ulifanywa kutokana na ongezeko kiwango cha wazee ukilinganisha na vijana katika jamii na lengo ni kuimarisha uchumi.
Lakini maafisa wamesema sera ya kuwa na mtoto mmoja katika familia itaendelea kutekelezwa hadi sharia ifanyiwe mabadiliko.
Mnamo Ijumaa, afisa mmoja alinukuliwa akisema kwamba wajawazito walio na mimba ya watoto wa pili hawataadhibiwa tena, jambo lililodokeza kwamba sera hiyo tayari ilikuwa imeanza kutekelezwa.
Lakini Jumapili Tume ya Kitaifa ya Afya na Upangaji Uzazi ilisema maafisa wa serikali wataendelea kutekeleza sharia hizo hadi sharia ifanyiwe marekebisho Machi.
"Sera ya kuruhusu watoto wawili sharti itekelezwe kwa mujibu wa sheria,” afisa wa tume hiyo alisema kupitia taarifa.
Hadi sera hiyo mpya iidhinishwe kisheria, maafisa wa serikali “lazima waendelee kutekeleza sera iliyopo sasa”, taarifa hiyo ilisema.
Serikali inakadiria kwamba familia 90 milioni zitapata nafasi ya kuongeza mtoto mwingine, sera ya kuwa na watoto wawili ikianza kutekelezwa.

Post a Comment

 
Top