Maafisa wanne wa
polisi wameshtakiwa baada ya kunaswa na kamera za siri (CCTV) wakimpiga
risasi na kumuua mshukiwa mmoja wa uhalifu
Gazeti mmoja la Afrika
Kusini, Sunday Times lilichapisha video hiyo iliyowaonesha maafisa hao
wakimpiga risasi na kumuua mshukiwa wa uhalifu licha ya kuwa alikuwa
amejisalimisha kwa polisi.Afisa mwengine wa polisi anaonekana akimvurumishia mateke katika tuko hilo lililotokea katika barabara ya Krugersdorp city, Magharibi mwa Johannesburg
Kwa mujibu wa gazeti la The Sunday Times, polisi walikuwa wakimfukuza Khulekani Mpanza kwa tuhuma za kutekeleza wizi wa mabavu tarehe 19 Oktoba .
Polisi walionekana kuwa wamembana na punde wakumuua.
Maafisa hao walijisalimisha wenyewe kwa mikono ya sheria baada ya nyuso zao kuonekana katika video hiyo.
Msemaji wa afisi ya kusimamia shughuli za Polisi IPD, Grace Langa, wanne hao watajibu mashtaka yanayowakabili baadaye leo.
Mbali na mauaji ya kinyama, wanne hao watashtakiwa kwa kuzuia haki isitendeke.
Picha hiyo inaonesha mshukiwa huyo akitupa Pistol yake kabla yake kunaswa na polisi na kuuawa.
Hili sio tukio la kwanza kuwakumba polisi nchini Afrika Kusini, Mwezi Agosti, maafisa wanane wa polisi walishtakiwa kwa kuua dereva wa teksi kinyama.
Walipigwa picha wakimfungia dereva mmoja wa teksi nyuma ya gari lao na wakaondoka huku akiburutwa barabarani hadi akafa.BBC
Post a Comment