Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam Mhe. Saidi Meck Sadiki akizungumza mbele ya wanahabari,
madaktari na baadhi ya akina mama waliokuwa na watoto waliozaliwa kabla
ya wakati maarufu kama Njiti (Hawapo pichani). Kushoto ni DoriS Mollel
ambaye ni Mwanzilishi na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Doris Mollel
Foundation (DMF) na wengine ni maafisa kutoka Hospitali ya Taifa
Muhimbili. (Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog).
Na Andrew Chale, Modewjiblog
[DAR ES SALAAM] Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepongeza juhudi binafsi
zinazofanywa na Taasisi ya Doris Mollel Foundation (DMF) katika harakati
zake za kusaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (njiti) na mambo ya
elimu hapa nchini huku ikiahidi kuendelea kushirikiana nayo kufikia
malengp yake.
Kauli hiyo imetolewa
mapema leo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Saidi Meck Sadiki
wakati wa kupokea vifaa maalum vya kusaidia watoto njiti vilivyotolewa
na taasisi hiyo ya Doris Mollel Foundation tukio lililofanyika katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jengo la Watoto.
“Tunatambua mashine hizi
ni bei kubwa na Serikali pekee yake haina pesa hivyo kwa kusaidiana na
wadau kama hivi n faraja sana na tunapongeza juhudi hizi za taasisi ya
DMF kwa kujitokeza kusaidia mashine kwa watoto njiti” ameeleza Mkuu wa
Mkoa huyo.
Mkuu wa Mkoa huyo
aliongeza kuwa, Mashirika mengine yaendelee kujitokeza kusaidia huduma
za kijamii ikiwemo vifaa kama taasisi ya Doris Mollel kwani asilimia
100 ya wagonjwa na watu wengine wenye mahitaji katika tiba wanakimbilia
Dar es Salaam hasa Hospitali ya Muhimbili.
“Tunaomba tena mukipata
nyingine musisite kutiletea hapa maana Mkoa huu unapokea wagonjwa wengi
kutoka maeneo mengi ya Tanzania na vifaa vya tiba mara nyingi vinakuwa
ni vichache, Huko mikoani wanapewa rufaa waanakuja hapa pia hivyo DMF
musisite kuja tena” alimalizia Mkuu wa Mkoa huyo.
Hata hivyo kwa upande wake
Mwanzilishi na mtendaji Mkuu wa DMF, Doros Mollel amemweleza Mkuu wa
Mkoa Meck Sadik kuwa wataendelea kushirikiana na Serikali bega kwa bega
katika juhudi za kusaidia watoto njiti nchini ikiwemo kutoa elimu,
vifaa na usaidizi kwa jamii dhidi ya kukabiliana na watoto njiti nchini.
Katika tukio hilo, Mkuu wa
Mkoa alishudia vifaa hivyo na kupokea kutoka DMF sambamba na
kutembelea wote ya watoto njiti pamoja na ile ya Kangaroo ambayo wamama
wenye watoto njiti wanakuwa wanapatiwa uangalizi maalum dhidi ya watoto
wao ikiwemo kupata joto la Mama na baadae alipanda mti maalum mbele ya
jengo hilo la Watoto kama kumbukumbu na juhudi za wadau katika kusaidia
jamii dhidi ya watoto njiti.
DMF imeweza kusaidia
vifaa katika wodi hiyo ya watoto Muhimbili vikiwemo (Suction machines,
Oxygen Concentrators na Feeding tubes). Aidha Doris Mollel amebainisha
kuwa baada ya hapo wanatarajia kuelekea mikoa ya Kanda ya Ziwa kutoa
vifaa kama hivyo huku lengo ikiwa ni kufika mikoa yote ya Tanzania.
Baadhi ya wafanyakazi
wa Hospitali ya Muhimbili wakishuhudia tukio hilo maalum la taasisi ya
DMF ilipotoa vifaa hivyo katika kitengo cha Jengo la Watoto.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Meck Sadik akipata maelezo juu ya vifaa hivyo vilivyotolewa na Taasisi ya DMF.
Msimamizi wa wodi ya
akina mama wanaopatiwa huduma ya Kangaroo dhidi ya watoto wao ambao
walizaliwa njiti, akimpatia maelezo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
alipotembelea wodi hiyo leo.
Picha ya juu na chini
Mkuu wa Mkoa wa Dar e Salaam akiwafariji baadi ya wakinamama
waliojifungua watoto kabla ya wakati maarufu njiti wakati alipotembelea
wodi hiyo ya watoto mapema leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam akimpatia zawadi ambayo ni jozi ya soksi kwa ajili ya kusaidia
watoto njiti kwa mmoja wa wamama waliokuwa katika wodi hiyo ya watoto
njiti.
Keki maalum iliyoandaliwa kwa ajili ya siku maalum ya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati maarufu njiti
Mtoto Amne Salim (3) ambaye ni njiti akikata keki maalum kwa niaba ya watoto wenzake katika tukio hilo mapema leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akimlisha keki mtoto Amne Salim katika tukio hilo.
Mtoto Amne Salim akimlisha keki Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Meck Sadik katika tukio hilo.
Baadhi ya akina mama
waliokwenye mpango maalum wa kutunza watoto wao waliozaliwa njiti
ujulikanao kama Kangaroo wakiwa wodini mapema leo wakati wa ugeni wa DMF
na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam walipotembelea wodi hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaamm Meck Sadik akipokea na kukabidhi vifaa maalum kwa ajili ya
kusaidia watoto njiti katika Hospitali ya Taifa Muhimbili vilivyotolewa
na Taasisi ya Doris Mollel Foundation mapema leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Meck Sadik akipanda mti maalum baada ya zoezi hilo la Taasisi ya
Doris Mollel Foundation kutoa misaada ya vifaa vya watoto njiti.
Shughuli hiyo ya upandaji mti wa kumbukumbu ikiendelea..
Mama mzazi wa Doris Mollel akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Post a Comment