0


SAFISHA SUMU MWILINI MWAKO NA UEPUKANE NA MAGONJWA TABIA

Napenda leo niongelee kwa kina kidogo kwa nini miili yetu inahitaji msaada wa kuiondolea sumu ili kurudisha utendaji kazi wake. Najua watu wengi wamelemewa na magonjwa sugu ambayo yameshindwa kujulikana ni magonjwa yanayotokana na nini,kwani kila uendapo hospitali wanakwambia huna ugonjwa na kuishia kuzifunika dalili za mwili kuzidiwa na sumu kwa kutumia dawa za maumivu, dawa za mzio ( allergey), dawa za usingizi, dawa za kubbost nguvu za kiume, dawa za uzazi wa mpango. Yote haya ni kwa sababu mwili wako
umelemewa na sumu na hutaki kuusaidia mwili wako kuondokana na hili.  Kama hujaungana na ukurasa wangu katika Facebook nakuomba ubofye like, DR BOAZ MKUMBO MD utakuwa unajipatia Makala zangu kila siku kupitia simu yako kiganjani.

Napenda niseme kuwa nia yangu ya dhati kwa nini hasa niliamua kuwa mtoa elimu hii ya afya na mwelimishaji namna gani tunaweza kuboresha afya zetu kupitia vyakula asili ni pale nilipo ona kuwa mfumo tunao tumia kutibu magonjwa ya dharura kama kuishiwa maji, malaria kali, ndio mfumo ule ule unatumika kutibu magonjwa sugu kama kisukari,vidonda vya tumbo,shinikizo la damu,uzito kupita kiasi,usaulifu,mzunguko mbovu wa hedhi,ugumba ,upungufu wa nguvu za kiume ndio maana magonjwa haya yamekuwa changamoto jinsi gani yanaweza kutibika kiurahisi kwa kutumia dawa za kisasa.

Nataka nikwambie kuwa kupitia mfumo mpya wa tiba siku zote huwa napenda kusema tiba asili ni tiba ambayo imeshushwa kiwango na kudharaulika sana kwa sababu bado watu hatujajua maslahi katika kazi pia yanatumika. Tiba asili napenda kuita kama Functional Medicine ndio tiba ya pekee yenye kulenga kuondoa chimbuko la tatizo na sio kuhangaika na kushusha dalili flani za ugonjwa. Basi nakupa uimara wa Fuctional medicine kupitia Makala hii, na kabla sijafika mbali napenda nirudie maelezo machache ambayo nilizungumzia katika Makala yangu ya kurasa zilizopita.

KUNA AINA NGAPI ZA SUMU AMBAZO ZINAWEZA KUULEMEA MWILI WAKO?
Hili ni swali ambalo wengi linawatatanisha sana basi leo ningependa ujifunze sina uhakika kuwa baada ya kujua haya machache utafurahia kuruhusu mwili wako uzidi kusumbuka na sumu nyingi kiasi hicho mwilini mwako.

1. Taka mwili zinazotengenezwa na shughuri zinaendelea mwilini mwako
Najua kuwa unafahamu kuwa mwilini mwako kuna mchakato wa shughuli mbalimbali ambao unaendelea bila kusitishwa maisha yako yote hadi pale kifo kitakapo kukuta.
TAFAKURI:

Basi chukua mfano kuwa una kiwanda chako cha kuchambua pamba na kusafirisha nchi za nje, basi kutakuwa na mbegu za pamba na makapi mengine yatapatiakana kutokana na mchakato huo, swali la kujiuliza utendaji kazi wa wafanyakazi wa kiwanda ndio watahitajika kuzitoa taka hizo kutoka mahali flani na kuziweka sehemu husika maana hazifai tena ndani ya kiwanda. Sasa basi kadri kiwanda kinavyokuwa kinatakiwa kiongeze wafanya kazi ili kuendelea kumudu utowaji wa taka kutoka ndani ya kiwanda na kuziweka mahali pake,endapo kisipokea hicho wale wafanya kazi wachache watalemewa na kazi na hatimaye kiwanda kitaharika kwani kitakuwa kichafu na chenye uhatari wa mlipuko wa magonjwa.

Mwili wako pia upo hatarini kwa sumu zinazopatikana kutokana na shughuli zinazoendelea mwilini mwako kila siku iitwayo leo! Mwili wako upo hatarini kupata mlipuko wa magonjwa sugu endapo usipochukua hatua sasa!

Watu wengi husema kuwa miili yetu imeumbwa na uwezo asilia wa kuondoa taka mwili zote zinazotokana na shughuli zinazofanyika mwilini mwako, Ndio hilo lina ukweli mkubwa sana kwani mwenyezi Mungu ameupa mwili wako mfumo makini sana wa utoaji taka mwili. Lakini tafiti zinaonesha kwamba kadri umri wako unavyozidi kuongezeka uwezo wa viungo vyako katika utendaji kazi katika utoaji taka mwili navyo hupunguza utendaji kazi wake!

Mfano, Figo ya kijana wa miaka 25 huwezi kulinganisha na figo ya mtu mzima mwenye miaka 50 kwani figo ya kijana wa miaka 25 bado ipo imara katika utendaji kazi wake kuondoa taka mwili zote kama urea, Kreatini na zinginezo kwa njia ya mkojo. Hivyo hivyo figo yam zee wa miaka 50 lazima utendaji kazi wako hupungua sana na unakuta figo haiwezi tena kuondoa urea vizuri na kreatini vizuri mwilini ambazo zote hizo ni taka mwili. Sasa unaposema miili yetu ina uwezo wa kuondoa sumu wenyewe ni kweli figo ya mzee wa miaka 50 hahitaji msaada kiutendaji? Ukweli ni kwamba miili yetu inafikia hatua inalemewa kutimiza utendaji kazi wake wa kuondoa taka mwili zote kutokana na viuongo vyetu vya utoaji taka na kusukuma damu na usambazaji damu hupunguza utendaji kazi wake kulingana na umri unavyo ongezeka. Najua unahitaji kuusaidia mwili wako, kwa nini usumbuke na kulemewa na maradhi kiasi hiki, leo safisha mwili wako!

2.Sumu zinazotoka kwenye mazingira ya udongo wenye sumu nyingi na hewa iliyochafuka.
Najua kuwa huwezi kuishi katika dunia hii kwa kujiepusha kugusana na arhi na vyote vilivyopo ndani ya ardhi n ahata hivyo huwezi kujizuia kuishi kwa kuvuta hewa ambayo imechafuliwa na utandawaza wa viwanda hapa duniani.

Kwa maana hio bidamu wote tupo hatarini sana wa kumiliki sumu zinazotokana na metali nzito kama Mercury ( haya ni madini ambayo hutumika sana kwa wingi kama Geita,nyamongo,katoro na sehemu zote zinazochimba dhahabu kwani hutumia madini haya kuosha dhahabu), madini mengine ambayo ni hatari kwa afya yako ni madini ya Lead, ambayo hupatikana kwenya mafuta ya betri za gari  na rangi za kupaka nyumba na vitu vingine.

Hizo ni baadhi ya metali nzito ambazo kila siku zinakufanya uwe mgonjwa rafiki yangu. Moja ya tafiti ambazo zilizofanyika hivi punde ilibainisha kwamba wagonjwa wengi wa mji wa Nyamongo walikuwa wanatibiwa kama malaria kutokana na dalili za kuchoka sana,mifupa kuuma,misuli kuuma na kichwa sugu kuuma ikiambatana na dalili zingine nyingi ndogo ndogo, walikuwa wakipima kipimo cha malaria bila kuona wadudu, lakini kwa sababu ya dalili zile zinashabiana na dalili za malaria basi walibiwa bila kujali kipimo cha malaria kuonesha hawana viini vya malaria.

Baada ya kuja kufanya uchunguzi Zaidi tafiti zilibaini kuwa wana sumu nyingi za mekyuli miilini mwao (mercury Intoxication) mercury unaweza kuipata hata katika kuchimba vyakula vya mizizi kama viazi,mihogo nk hivyo basi sio kwamba ujiepushe na mahusiano yako na mazingira wakati wa kazi yako, bali hakikisha unausaidia mwili wako kuondoa sumu hizi ambazo mwili unalemewa kwani kiwango cha sumu kinazidi sasa utendaji kazi wa miondoa sumu hizi miilini mwetu.

Inaweza kuwa hata wewe umedhoofika kiafya kutokana na sumu za metali nzito kama hizi, au kutokana na madawa mbali mbali ambazo umekuwa ukitumia katika kilimo chako kama viua wadudu na vimekuathiri na unakabiliwa na dalili zisizo za msingi sasa , unahitaji kupunguza sumu hizo kuusaidia mwili wako kuondoa kabisa sumu mwilini mwako na kurudisha utendaji kazi wa mwili wako.


3. Sumu zitokanazo na mionzi mbalimbali.
Mionzi katika ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia huwezi kuepukana nazo hata kidogo rafiki,kwani dunia imejaa vifaa vinavyotoa mionzi mikali na hafifu. Mbali na hivyo kila kona miamba imekuwa ikichokozwa na kusababisha mionzi mizito ya madini mazito kuanza kutoka na hatimaye kuathiri utendaji kazi wa mwili wako.
Hivyo basi ni jukumu lako kupambana na mionzi hii kwa kuusadia mwili wako kuondoa kabisa

Baada ya kujadili mambo hayo machache sasa umefahamu kwa nini mwili wako unalemewa na sumu na unahitaji msaada wako hebu zitambue dalili za watu wengi wenye matitizo yatokanayo na mwili kulemewa na sumu mwilini.

1. Tatizo sugu la choo kigumu (constipation)
2. Kichwa kuuma kwa muda mrefu,msongo wa mawazo,hasira za mara kwa mara,ukosefu wa usingizi nk
3. Misuli kuuma sana na uchovu usio ambatana na dalili za msingi za magonjwa ambukizi kama malaria UTI nk
4. Tumbo kujaa gesi
5. Vichocheo vya kike kuvurugika na kupelekea kupata ugumba
6. Kukosekana na nguvu za kiume
7. Kutopungua uzito hata pale unapukuwa unafuata mlo sahihi
8. Sukari,presha kutoshuka bila kujali upo kwenye matibabu
9. Allergy na vyakula mbalimbali na mafua ya muda mrefu
10. Magonjwa sugu ya ngozi kama pumu ya ngozi,psoriasis,vertiligo nk
Inaweza kuwa hauna dalili hizo lakini ni busura kujua kuwa upo katika mazingira hatarishi na inaweza kuwa ukawa na kiwango flani cha sumu hizi ambapo kiwango tu kinachohitajika kuleta dalili hakijafikiwa,kikifikiwa dalili utaziona.

Hebu leo napenda nikupe suluhisho la kujiepusha na ulimwengu wenye sumu nyingi kutoka kila kona inayokuzunguka mpendwa, hebu leo nakupa siri ya wengi ambao wamekuwa wakiusaidia mwili wao kusafisha sumu ambazo mwili umelemewa. Napenda urejee maelezo yangu haya hapa,kma ukiona itakufaa program hii nakuomba ushiriki rafiki ujiepushe na maradhi haya.

60 DAYS CLEANSE PACKAGE FOR DETOXICATION
Napenda kukupa program hii ambayo nimeanzisha siku nyingi sana baada ya kupata shuhuda mbalimbali wakishukuru kuwa Dr Boaz Mkumbo  nilikuwa ni mtu ambaye sipati hata usingizi lakini sasa Napata usingizi na misuli yangu imetulia kabisa.

Basi ni zamu yako kuniletea ushuhuda kupitia elimu hii unayo ipata rafiki yangu kuanzia sasa endapo tu ukiamua kuitumia kwa kuboresha afya yako na kujua kuwa mwili wako umelemewa usiacha na kusubili uanze kutoa malalamishi kupitia dalili kama nilivyozitaja hapo juu,  utakuwa umechelewa!

Kiufurushi hiki cha siku 60 ambacho kitakubali maisha yako kutoka kwenye kuumwa hadi furaha ya afya bora ndani ya siku 60. Najua utafurahia kufikia hapo,kama wengine walipofikia! Kifurushi hiki kimegawanywa katika matibabu ya aina mbili kama ifuatavyo,

1. COLON CLEANSE( KUSAFISHA UTUMBO MPANA)
Hii ni huduma utakayo ipata kwa kutumia virutubisho asili ambavyo vitakusaidia kuondoa sumu zote katika mfumo wa chakula na kuponyesha mfumo wa chakula ambao umeharibika kwa muda mrefu.
Pia utajipatia kirutubisho ambacho kitarudisha madini yote muhimu mwilini mwako ambayo yanakuwa hayawezi kufyonzwa na utumbo umwembamba ambayo ulikuwa umeharibika, hivyo tunarudisha uhalisia wa mwili wako kuunguza mafuta na kuendesha shughuli zote za mwili kwa kukuongezea madini ya selenium,zinc,manganese ambazo ni catalyst nzuri sana katika shughuri zote zinazofanyika mwilini mwako, pia utajipatia lishe ya kutosha ndani yake ili uweze kufurahia maisha ya afya yako yenye ulinzi thabiti.

2. MATIBABU YA KUONDOA MIONZI MIBAYA NA MAUMIVU YA MISULI YA MUDA MREFU
Kwa wale ambao wamekuwa wakisumbuka na tatizo la misuli kwa muda mrefu, kuuma sana bila kutumia dawa za maumivu huwezi kupata usingizi basi hii ni program itakufaa kwa ajiri yako rafiki. Utapewa matibabu kwa muda wa wiki 4 ambayo yatalenga hasa kukuondoa maumivu yote ya misuli,mgongo,msongo wa mawazo,presha kuwa juu bila kujali umekunywa dawa,sukari haishuki huku upo kwenye dawa, basi tutashughurikia tatizo hilo na utarudi katika hali yako hakika ndani ya wiki moja ukiwa unaendelea na tiba.  Sio machache hayo tu niliyo andika utanufaika na program hii inayotolewa na mimi bali utajipatia mengi hata ambapo nikitaka hapa sitaweza kumaliza. Huduma hii utaipata kwa kuhudhuria kwenye matibabu kwa muda wako maalumu ambapo utakuwa na nafasi kwani tumepangilia huduma hii kwa kutumia mashine za kisasa na zenye uwezo wa juu sana kutimiza malengo yako kiafya.

Napenda nihitimishe kwa kushukuru kusoma Makala hii, na nitakukaribisha utufikie kiofisi uje upajipatie huduma hii, kuepusha magonjwa ambayo hayana msingi mwilini mwako.

Post a Comment

 
Top