0
 John
Marekani bado inachunguza kubaini iwapo ameuawa
Wanajeshi wa Marekani wametekeleza shambulio la kutoka angani lililomlenga mwanamgambo wa Islamic State kutoka Uingereza ajulikanaye kama "Jihadi John", Pentagon amesema.
Mohammed Emwazi, Mwingereza aliyezaliwa Kuwaiti, alilengwa kwenye shambulio hilo lililotekelezwa karibu na mji wa Raqqa, nchini Syria.
Msamo mkali wa kumtafuta Emwazi ulianza baada ya mwanamgambo huyo kuonekana katika video akiwakata shingo mateka wa kutoka mataifa ya Magharibi.
Pentagon bado inachunguza kubaini iwapo Emwazi ameuawa kwenye shambulio hiyo.
Afisa wa habari wa Pentagon Peter Cook amesema: "Tunatathmini matokeo ya operesheni ya leo usiku na tutatoa taarifa zaidi baadaye.”
Emwazi anaaminika kusafiri Syria 2013 na kisha akajiunga na wapiganaji wa Islamic State.
Alionekana mara ya kwanza kwenye video Agosti mwaka jana, kanda ya video ilipopakiwa mtandaoni ikionyesha mauaji ya mwanahabari wa Marekani James Foley.
Baadaye alionekana kwenye video za kuuawa kwa mwanahabari wa Marekani Steven Sotloff, mfanyakazi wa shirika la kutoa misaada wa Uingereza David Haines na dereva wa teksi kutoka Uingereza Alan Henning.
Aidha, alikuwepo kwenye video ya kuuawa kwa mfanyakazi wa kutoa misaada kutoka Marekani Abdul-Rahman Kassig, aliyejulikana pia kama Peter na mwanahabari wa Japan Kenji Goto.
Katika kila video, alionekana akiwa amevalia kanzu nyeusi na barakoa nyeusi ya kufunika uso wake.
Awali alijulikana tu kama "Jihadi John", lakini baadaye ikabainika kwamba alikuwa ni Emwazi, kutoka magharibi mwa London, Februari.

Post a Comment

 
Top