Hospitali kuu ya Muhimbili nchini Tanzania,imesema kwamba mashine ya MRI imeanza kufanya kazi tena baada ya kurekebishwa.
Taarifa
ya hospitali hiyo imesema kuwa kifaa hicho kimeanza kufanya kazi huku
vifaa vyengine kikiwemo kile cha CT-Scan kikendelea kurekebishwa huku
hospitali hiyo ikitarajiwa kutoa tamko lake kwa vyombo vya habari siku
ya Alhamisi.''Tunaomba radhi kwa matatizo waliyopata wagonjwa ambao walikuwa wanafanyiwa uchunguzi na kifaa hicho'',ilisema taarifa hiyo iliotiwa saini na mkuu wa mawasiliano bwana Aminiel Aligaesha.
Kulingana na gazeti la The Citizen nchini Tanzania, urekebishaji wa kifaa hicho unafuatia ziara ya kushtukiza iliofanywa na rais John Pombe Magufuli siku ya Jumanne ambapo aligundua kwamba kifaa hicho cha CT-Scan kilikuwa hakifanyi kazi kwa kipindi cha miezi miwili swala linalowaweka wagonjwa katika mlolongo mrefu.
Rais Magufuli aliuagiza usimamizi wa hospitali hiyo kuhakikisha kwamba kifaa hicho kinarekebishwa kwa haraka iwezekanavyo.
Wakati wa ziara hiyo rais Magufuli alimuondoa kaimu mkurugenzi wa hospitali hiyo Dokta Hussein Kidanto na kuivunja bodi ya taasisi hiyo.
Post a Comment